ANGALIA JINSI MWANAJESHI AMLAZIMISHA RAIA KUOGELEA KWENYE MAJI YALIYOTWAMA BARABARANI KARIAKOO


Picha unazoona sio utani wala sinema ni raia wa kawaida akiogelea kwenye dimbwi kwa amri ya mwanajeshi.
Raia huyo alikutana na adhabu kali za mwanajeshi huyo baada ya kukutwa amevaa mavazi halisi ya jeshi la Tanzania maeneo ya Kariakoo Dar es Salaam.

Jamaa huyo alipokamatwa na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha akaamriwa kuvua mavazi hayo na kisha kuaza kutumikia mazoezi ya hatari ..
Haya mavazi raia wanayapenda ila kwenda kutumikia jeshi hawataki ...ahahaaa jamaa alichokipata hawezi kutamani nguo za rangi ya kombat maisha yake yote.

Read more >>
widgets for blogger

GARI AINA YA BMW ALILOTUNZWA WEMA NA MENEJA WAKE NI UTATA MTUPU

Achana na lile gari aina ya Nissan Murano alilozawadiwa na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, gari lingine aina ya BMW 545i aliloletewa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kwenye pati ya ‘bethidei’ yake ni utata mtupu na maswali kibao.
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akiwa ndani ya Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa na meneja wake.
NYUMBANI KWA MADAM
Pati hiyo ambayo iliandika historia katika ulimwengu maridhawa wa mastaa iliangushwa nyumbani kwa mwanadada huyo, Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar, wikiendi iliyopita ambapo alitimiza umri wa miaka 26.
Katika shughuli hiyo, waalikwa ambao sehemu kubwa walikuwa watu wenye majina, walikula na kunywa kuanzia mchana hadi usiku mnene.

NISSAN MURANO
Akiwa Marekani, Diamond alimuagiza mama yake, Sanura Kassim ‘Sandra’ apeleke gari aina ya Nissan Morano lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 36 za madafu ikiwa ni zawadi ya jamaa huyo kwa mkewe huyo mtarajiwa.

Gari aina ya BMW 545i alilozawadiwa Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na meneja wake.
Alipoliona gari hilo, Wema alipigwa na butwaa huku akimshukuru Diamond ambaye kwa sasa amempachika jina la Chibu baada ya lile la Dangote ‘kueksipaya’.
MANENO KUNTU
Huku akiambatanisha na picha ya gari hilo, kupitia ukurasa wake wa Instagram alimwandikia Wema: “Nilitazama nikupe vingi huenda ingesaidia kukueleza ni kiasi gani napenda nikuone ukiwa umefurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa...lakini tu sina uwezo huo Mumy...tafadhali pokea hicho kidogo hiki nilichojaliwa leo.”

BMW UTATA MTUPU!
Gari aina ya BMW alilokabidhiwa na meneja wake, Martin Kadinda ndilo habari ya mjini huku nyuma yake kukiwa na maswali kibao.

Martin Kadinda akionyesha funguo ya Gari aina ya BMW aliyomzawadia Wema.
MAMA WEMA AHOJI
Wa kwanza kuhoji alikuwa ni mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu ambaye alikataa kwamba Kadinda hawezi kutoa zawadi ya gari kama hilo hivyo minong’ono ikawa ni mingi.
Baada ya kuona hivyo, Kadinda alitoa kadi ya gari hilo lenye namba spesho za usajili ambapo jina la mmiliki lilisomeka Wema Sepetu.

MKONGO ATAJWA
Hata hivyo, pamoja na utetezi wake, maneno yaliendelea kusambaa kama moto wa kifuu kwamba nyuma ya gari kuna stori kubwa inakuja.

Muonekano wa keki ya ‘bethidei’ ya Wema.
Minong’ono mingine ilikwenda mbele zaidi huku jamaa mmoja mfanyabiashara kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (Mkongomani) akitajwa kulinunua na kumpa Kadinda akakabidhi.
Baada ya kuona gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 56 za madafu zinaleta utata, kama kawaida yake, Kadinda alikimbilia kwenye ukurasa wake wa Instagram akaandika:

“....Gari hili linatokana na kazi ndogo tuzifanyazo na sapoti kubwa ya watu wanaotutakia mema. Peke yangu nisingeweza bila sapoti yao....”
Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akimlisha keki mama yake.
MSISITIZO
Akizungumza na gazeti hili juu ya sakata hilo, Kadinda alisema kwa msisitizo: “Ni mimi ndiye nimemnunulia Wema hilo gari.”

MASWALI
Huku Kadinda akisisitiza hivyo, waalikwa walibaki na maswali vichwani likiwemo lile linaloulizwa zaidi kwamba iweje yeye (Kadinda) aendeleshe gari la thamani ndogo aina ya Toyota Corola halafu ampe Wema BMW?
“Hapa pana kitu na kitakapobumburuka itakuwa soo, ni bora Kadinda angefunguka ukweli kuliko kuja kunyooshewa vidole baadaye, ngoja tusubiri,” alisikika mmoja wa mastaa walioalikwa (jina kapuni).

Akimlisha keki mamamkwe wake.
MENGINE YATOKANAYO
Pati hiyo ya Wema iligawanyika mara mbili ambapo ya kwanza ilianza saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 huku nyingine iliyohusisha watu maarufu ikianza baadaye hadi ‘kokoriko’.

KEKI 69 MEZANI
Katika hali isiyo ya kawaida, sherehe hiyo ilikuwa na keki zipatazo 69 ambazo zililetwa na baadhi ya mastaa ambao walihudhuria sherehe hiyo huku kukiwa na vinywaji vya kufa mtu (wiski tu), loko bia tupa kule.

Akimlisha keki Jokate.
NDAFU
Kwa upande wa nyama kulikuwa ndafu mzima ambaye watu walimtafuta hadi wakasaza.

MAMA DIAMOND AMTANGAZA RASMI MKWEWE  
Katika sherehe hiyo, mama Diamond alipopewa kipaza sauti ‘maiki’ ili anene chochote alisema kuwa Wema ni mkwe wake wa halali na kwamba anampenda hivyo asiwe na wasiwasi kwani hakuna mkwe mwingine atayatokea zaidi yake.

Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ akifungua shampeni kwaajili ya shughuli hiyo.
“Jamani huyu ndiye mkwe wangu, Mrs Chibu (Diamond) ndiye mkwe wangu hasaaa...,” alisema mama Chibu huku watu wakishangilia.
MILIONI 10
Kwa mujibu wa Kadinda, shughuli hiyo iligharimu zaidi ya Sh. milioni 10 hadi kukamilika na kuonekana ya tofauti na pati nyingine za mastaa Bongo.

Wema akiongea jambo kabla ya kukata Ndafu.
AMWAGIWA NOTI
Ulipofika muda wa kutunzwa zawadi, watu walijitokeza kumtunza Wema fedha ambazo hazikuweza kupatikana kiasi chake mara moja huku staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiweka rekodi kwa kumwaga ‘minoti’ mingi katika hafla hiyo.
Read more >>

SHEHE: AUNT EZEKIEL HANA NDOA KWA SABABU ANAMNYIMA MUMEWE UTAMU, SOMA ZAIDI HAPA.

SHEIKH Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa ameweka wazi kuwa msanii nyota wa filamu, Aunt Ezekiel ambaye aliolewa na Sunday Demonte hana ndoa kutokana na kukaa mbali na mumewe kwa zaidi ya miezi sita.
Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa akizungumza jambo.
“Hakuna ndoa kati ya mtu yeyote ambaye amezidi miezi 6 bila kukutana na mumewe kwa mujibu wa dini ya kiislamu.
Msanii nyota wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel
“Kwa kawaida mwanamke ambaye hajakutana na mumewe kwa miezi 6 au zaidi baada ya ndoa yao, hupaswa kwenda mara moja Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kulalamika na hatimaye kudai talaka, ikiwa mwanamke ameridhika na hali hiyo, naye akaamua kukaa kimya huku akifanya mambo yake na kuanzisha uhusiano na wanaume wengine maana yake amejitoa mwenyewe kwenye mamlaka ya mumewe, hivyo hapo kunakuwa hakuna ndoa tena,”alisema Shehe.
Read more >>

UKATILI: MEYA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MKEWE



Daniel Crespo enzi za uhai wake.
MEYA wa Bell Gardens, California nchini Marekani, Daniel Crespo ameuawa jana kwa kupigwa risasi na mkewe nyumbani kwake.
Crespo alipigwa risasi wakati wa mzozo baina yake na mkewe ambapo mtoto wao wa kiume mwenye miaka 19 alijaribu kuingilia na kusukumwa na baba yake ndipo mtuhumiwa alipofyatua risasi.
Marehemu alipoteza maisha akiwa njiani kupelekwa katika hospitali iliyo karibu na nyumbani kwake.
Mke wa marehemu,  Levette Crespo anashikiliwa na polisi kwa tukio hilo. 
Read more >>

BIFU LA FLORA, NISHA LAFIKA SEHEMU MBAYA ZAIDI.

WASANII wawili waliowahi kuwa marafiki wa kupika na kupakua, Flora Mvungi na Salma Jabu ‘Nisha’ bifu lao sasa limefika pabaya baada ya hivi karibuni kuwaacha watu midomo wazi kwa kitendo chao cha kupitana kama hawafahamiani.
Msanii wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’.
Ishu hiyo ilitokea wikiendi iliyopita kwenye sherehe ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya staa wa filamu, Wastara Juma iliyofanyika katika ukumbi wa Dar West uliopo Tabata jijini Dar es Salaam. Wawili hao walikutana mlangoni wakati wa kuingia, lakini Flora alimpita Nisha kama hamfahamu na kama hiyo haitoshi, walipoingia ndani, kila mmoja alikaa meza yake.
Wakati sherehe zikiendelea, ukafika wakati wa kufungua shampeni na baada ya tukio hilo, Nisha alipewa jukumu la kuwagawia wageni waalikwa kwa kuwamiminia kwenye grasi zao, lakini alipofika kwenye meza aliyokaa mwenzake, Flora alikataa glasi yake kuwekwa kinywaji hicho.
Msanii wa filamu Bongo, Flora Mvungi.
Baada ya tukio hilo, paparazi wetu aliwafuata mastaa hao na kuwauliza kulikoni, na Flora alisema: “Sikumuona Nisha mimi, na shampeni nimekataa kwa sababu huwa siipendi.”
Kwa upande wake, Nisha alisema: “Mimi sikumuona Flora, kuhusu Shampeni mbona nilimimina kwenye glasi zote jamani!”
Read more >>

FUMANIZI: SERENGETI BOY NA MKE WA KIGOGO WAFUMANIWA WAKIWA GEST WAKIJIANDAA KUFANYA NGONO

Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine (24), mkazi wa mtaa wa Kitangiri jijini Mwanza amenaswa ‘live’ gesti akiwa na mke wa kigogo mmoja (jina kapuni), aitwaye Mwanaidi wakijiandaa kuvunja amri ya sita.
Baada ya fumanizi kati ya Serengeti boy aliyefahamika kwa jina la Marck Costantine na mke wa kogogo.
Tukio hilo lilijiri Septemba 18, mwaka huu kwenye gesti moja maarufu iliyoko mitaa ya Kitangiri baada ya kigogo huyo kupewa ‘ubuyu’ kwamba anaibiwa mali yake ndipo akaandaa mtego na kufanikiwa kumnasa kijana huyo alipokutwa kwenye chumba namba 4 cha gesti hiyo akijiandaa kuserebuka.
“Kigogo alipopewa mchoro huo na wambea, siku ya tukio alimshtua Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitangiri, Maginga Patroba, wakatia timu katika gesti hiyo, wakawakuta wachepukaji hao wakiwa kitandani huku Marck akiwa tayari ameshachojoa nguo, Mwanaidi akiwa bado,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
Akisainishwa kulipishwa faini.
“Kigogo aliamuru wahudumu wagonge mlango ili wahusika wasishtuke, walipofungua ndipo mwenyekiti sabamba na kigogo huyo wakazama ndani.”
Mwanaidi alipoona flashi za kamera ya mapaparazi zikiwamulika, alianza kuangua kilio mbele ya mumewe kumuomba awasamehe lakini kigogo huyo alimtaka kijana huyo amlipe fidia ya shilingi milioni moja kama adhabu ya kutembea na mke wake.

Kutokana na hali ya uchumi ya kijana huyo kutokuwa nzuri, hakuweza kulipa kiasi hicho cha pesa badala yake aliomba kupewa muda wa kulipa pesa hizo.Barua ya makubaliano ya kulipwa pesa kwa kigogo huyo shilingi laki tano.
Chini ya uangalizi wa mwenyekiti, Marck aliandika barua ya makubaliano jinsi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa kwa kigogo huyo na iwe kama fundisho kwake kuachana na tabia za kutembea na wake za watu.
Kwa upande mwingine, mwenyekiti Patroba alikiri kumfahamu Marck na kudai ni kijana wa mtaani kwake na kumuonya asirudie mchezo huo mchafu.
Mke huyo wa Kigogo aliyefahamika kwa jina moja la Mwanaidi akiwa analia akiomba msamaha kwa mumewe.
“Namfahamu huyu kijana nimeshangazwa na kitendo hiki anachokifanya kwani ni vitendo ambavyo havikubaliki katika jamii hivyo kama kiongozi wa mtaa huu nitaendelea kutoa ushirikiano ili kuukomesha tabia kama hizi za kuvunja miji ya watu,’’ alisema Patroba.
Read more >>

CHELSEA YANG'AA, PSG YAIBANJUA BARCELONA,, PATA MATOKEO HAPA ZAIDI


CHELSEA imepata ushindi wa ugenini katika Ligi
ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Sporting
Lisbon ya Ureno bao 1-0, wakati Manchester City
imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Roma
ya Italia usiku huu.
Katika mchezo wa Kundi G, bao la Nemanja
Matic dakika ya 34 limemfanya kocha Jose
Mourinho aitambie timu ya nchini kwake,
Sporting.
Uwanja wa Etihad, Sergio Aguero alitangulia
kuifungia City kwa penalti dakika ya nne kabla ya
mkongwe Francesco Totti kuisawazishia Roma
dakika ya 23 katika mchezo wa Kundi E.
Bao pekee la Thomas Mueller dakika ya 22
limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0 ugenini
dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika mchezo
mwingine wa Kundi E. mchezo mwingine wa
kundi hilo usiku huu, Schalke 04 imelazimishwa
sare ya 1-1 nyumbani na Maribor.
Kundi F, PSG imeichapa FC Barcelona mabao 3-2,
mabao yake yakitiwa kimiani na David Luiz
dakika ya 10, Marco Veratti dakika ya 26 na
Blaise Matuidi dakika ya 54, wakati mabao ya
wageni yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 12
na Neymar dakika ya 56.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo, APOEL Nicosia
imelazimishwa sare ya 1-1 na Ajax nyumbani bao
la wenyeji likifungwa na Manduca dakika ya 31
na la wageni likifungwa na Lucas Anderson
mapema dakika ya 28.
Kundi H, BATE Borisov imeichapa 2-1 Athletic
Bilbao nyumbani mabao ya washindi yakifungwa
na Denis Polyakov dakika ya 19 na Karnitskiy
dakika ya 41, wakati bao la wageni lilifungwa na
Aritz Aduriz dakika ya 45.
Shakhtar Donetsk imelazimishwa sare ya 2-2
nyumbani na FC Porto, mabao ya wenyeji
yakifungwa na Alex Teixeira dakika ya 52 na Luiz
Adriano dakika ya 85, wakati ya wageni yote
yamefungwa na Jackson Martinez dakika ya 89
kwa penalti na 90.
Read more >>

UMOJA WA MA-GIRLFRIEND WAMEKUJA NA HII BAADA YA DIAMOND KUTOA ZAWADI YA GARI KWA WEMA


zawadiSeptember 26 ilikua ni siku ambayo mrembo kutoka Tanzania Wema Sepetu alisherehekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ndani ya siku yake hii ukitoa party aliyoifanya kulikuwa na vitu mbalimbali vya kuvutia.
Siku hiyo Diamond platnumz aliamua kumzawadia zawadi ya gari mpenzi wake Wema Sepetu gari aina ya Nissan Murano ambapo alipost instagram na kuandika maneno yafuatayo yaliyoambatana na picha ya zawadi hiyo.
zawadi
msgMbali na zawadi aliyoitoa Diamond Platnumz ya gari hilo pia Meneja wake Martin Kadinda nae alimpatia Wema Sepetu zawadi ya Gari aina ya BMW mpya kabisa ikiwa na namba mpya za sasa.
bmw
Sasa baada ya zawadi hizo kuonekana eti umoja wa Ma-Girlfriend Tanzania nao wameamua kutoa Ya moyoni kwa Ma-Boyfriend wao kuhusu birthday zao inapofika muda wa kusherehekea,hiki ndicho walichokiandika.
www
Read more >>

ONA SELFIE ZA WOLPER....AKIWA NDANI YA KIVAZI HATAREEEE.

Read more >>

BONGO HUYU MTOTO KAUMBIKA BALAA, MUONE HUYU

Read more >>

SABABU YA WAGANGA KUWAFANYA WATU WENGINE KUWA MATAJIRI NA WAO KUBAKI MASKINI..!! SOMA HAPA

Kuna watu ambao wanapata mafanikio makubwa kwa kutumia uchawi. Ila mafanikio yale hayaletwi na uchawi bali imani ya mtu husika.

Tutajadili kwa nini waganga wanaweza kuwapatia watu wengine dawa au mbinu za kuwa matajiri wakati wao ni masikini. Na pia tutaangalia jinsi ambavyo unaweza kutumia mbinu hizi wanazotumia waganga bila ya wewe kuwa mchawi na ukafikia mafanikio makubwa.

Kila mmoja wetu anaelewa kwamba kuna watu wanakwenda kwa waganga na wanasaidiwa kupata utajiri. Japokuwa utajiri huu haudumu, lakini angalau wanaupata kwa kiwango fulani.

 Wakati waganga hawa wanawasaidia watu kuweza kujenga magorofa, wao bado wanakaa kwenye vibanda vya nyasi.

Sasa kwa nini wao wasingetumia uchawi wao na kuwa matajiri zaidi ya hao wateja wao? Ina maana wao hawapendi utajiri huo?

Mbinu za waganga kuwasaidia watu kupata utajiri.
Watu wanaokwenda kwa waganga ili kupata utajiri au mafanikio yoyote hupewa masharti ambayo ni magumu kwa kiasi fulani. 

Na watu hawa huambiwa wakivunja masharti hayo tu utajiri wao unaisha mara moja. Ni masharti haya ambayo humjengea mtu nidhamu kubwa sana na kumfanya aweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa kuliko wengine ambao wanafanya anachofanya. 

Kwa mfano mganga anamwambia mtu kila siku aamke asubuhi na mapema sana na apasue nazi barabarani ndio aende kwenye biashara zake. 

Kupasua nazi hakuna uhusiano wowote na mafanikio yake ila kuamka asubuhi na mapema kila siku ina msaada mkubwa kwenye mafanikio yake.

Hivyo mtu huyu atafuata masharti haya kila siku na hata kama kuna siku hajisikii itambidi afanye tu kwa sababu ameshaaminishwa akiacha atafilisika.

Sasa wewe ambaye huna sharti la aina hii siku ukiwa hujisikii vizuri unalala, siku nyingine unachelewa na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa. 

Masharti mengine kama kutokufanya starehe, kutokunywa pombe, kuvaa nguo moja na mengine mengi yanapelekea mtu kupunguza matumizi na kupata muda mwingi wa kufikiria kazi au biashara yake.

Masharti mengine yanayotolewa na waganga ni kumfanya mtu aweze kuondoka kwenye woga wake(comfort zone). Kila mmoja wetu kuna vitu fulani anaogopa kufanya, lakini vitu hivi ndio vinaweza kumletea mafanikio.

 Ili kukuondolea woga huu mganga anamfanya mtu afanye jambo kubwa sana ambalo litamuondolea woga kabisa.

 Kwa mfano mtu anaambiwa aue, kwa kuona kwamba ameweza kuua mtu, inamfanya mtu asizuiwe na kitu chochote.

Kikubwa ambacho mganga anamsaidia mtu ni kumjengea utaratibu ambao lazima kila siku ataufuata na pia kumjengea nidhamu binafsi na hivyo kuweza kufanya jambo hata kama hajisikii kufanya. Na hili ndio hitaji kubwa la kuweza kufikia mafanikio.

Kwa nini waganga hawawezi kutumia mbinu hii wenyewe.?
Kwa sababu wanajua inavyofanya kazi na pia hawana mtu wa kuwajengea imani hiyo kubwa kwao wenyewe.

Kwa nini watu baadaye hufilisika?
Wengi hufilisika baadae kwa sababu wanapopata mafanikio wanasahau kutumia yale masharti waliyopewa na pia imani yao inakuwa imewekwa kwenye vitu fulani(mfano hirizi) badala ya kuwa kwao wenyewe.

Ufanyeje ili uweze kutumia mbinu hii kufikia mafanikio.
Cha kwanza kabisa lazima ujijengee nidhamu binafsi. Jiwekee masharti yako ambayo utayafuata kila siku na hakikisha unayafuata.

Kwa mfano weka utaratibu kwamba kila siku utakuwa unaamka saa kumi asubuhi, kuipanga siku yako na kisha kujisomea kidogo. 

Baada ya hapo unawahi kwenye eneo lako la kazi au biashara na kuanza kazi zako mapema. Pia unaweza kujiwekea utaratibu kwamba kila mteja au mtu yeyote unayekutana naye kwenye siku husika atajisikia vizuri kukutana na wewe.

Fuata masharti haya kila siku na utaona mabadiliko makubwa kwenye maisha yako na shughuli zako.

Kwa hiyo mpaka sasa una mbinu mbili za uhakika za kufikia mafanikio;
1. Una uwezo mkubwa uko ndani yako, ila unatakiwa kuwa na imani kubwa sana kwamba unaweza kupata kile unachotaka.

2. Lazima uwe na nidhamu binafsi, uwe na masharti(rituals) na uwe na utaratibu wa kufanya kila siku (routine). Vitu hivi jiwekee mwenyewe na vifuate kila siku kwenye maisha yako.

Ukiweza kufanya mambo hayo mawili ni lazima utafikia mafanikio makubwa.

Nakutakia kila la kheri katika kufikia mafanikio. Kumbuka unaweza kufanikiwa kwa kiwango kikubwa sana bila ya kutumia uchawi au kwenda kwa mganga.Uchawi kamili upo kwenye kichwa chako. Anza kuutumia sasa.

Read more >>

NILISHUHUDIA KWA MACHO YANGU NIKICHOMWA MOTO

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Richard Osward (40) mkazi wa Tabata Segerea, hivi karibuni alinusurika kuuawa kwa kuchomwa moto na wananchi baada ya kuhisiwa kuwa mwizi alipokutwa alfajiri akiwa na mfuko ambao ndani yake kulikuwa na bomba, huko Segerea.
Richard Osward aliyechomwa moto na watu wenye hasira kali akidhaniwa kuwa ni mwizi.
Akizungumza kwa shida akiwa katika wodi namba 23 iliyomo ndani ya Jengo la Sewa Haji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Richard alisema tukio hilo lilimkuta akiwa ameongozana na rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Moses na kwamba walikuwa wakielekea Gerezani, Kariakoo ambako wanajishughulisha na ufundi wa magari.
Akiuguza majeraha ya moto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Nilitoka nyumbani nikiwa nimebeba bomba katika mfuko nikitaka kwenda kuliuza, tulipofika Segerea Seminari, tulisimamishwa na watu ambao walitutilia shaka wakaanza kutupekua.
“Wakasema sisi ni wezi na hivyo lazima watuadhibu. Mara akapita dereva wa bodaboda ambaye alishinikiza kuwa sisi ni wezi na kutaka wachange hela wakanunue petroli ili watuchome moto, uzuri ni kwamba kwa kuwa ilikuwa usiku,wakashindwa kupata hayo mafuta,
lakini tunashukuru dada mmoja alikuja amevaa sare za kampuni moja ya ulinzi, akatukingia kifua na kusema watupeleke polisi na ndiyo tukafikishwa Kituo cha Polisi cha Stakishari na baadaye kunileta hapa kwa matibabu, kilichoniponza ni njaa lakini mimi ni mtu safi katika jamii, mwenzangu alifanikiwa kukimbia.”
Read more >>

HUYU NDIO ALIYEMPA WEMA BMW NA SI DIAMOND

Baada ya Diamond Platnumz kumpa wema gari aina ya Nissan Murano kama zawadi ya siku yake ya kuzaliwa basi maswali mengi yamejitokeza kuhusiana na mtu aliyemkabidhi wema gari aina ya BMW neupe huku kila mtu akitaja mtu wake lakini leo aliyemkabidhi gari hiyo, manager wake, Martin Kadinda amefunguka haya…

 
HATARI SANA: HII NDIO ZAWADI MAALUM YA DIAMOND KWA WEMA SEPETU IKISINDIKIZWA NA UJUMBE MTAMU WA KIMAHABA!hii ndio aliyopewa na Diamond

Yes…. Not only Murano from ya baby @diamondplatnumz this BMW is yours yes…. Suprised kuona jina kwa kadi?? I meant it… this car came from kazi ndogo tufanyazo na support kubwa ya watu who wish you the best always… peke yangu nisingeweza bila support yao. One thing you should know nimejitolea kufanya kazi na wewe because naamini kwa tanzania ur my number one celebrity and my wish is to see u living as a truly superstar…. Make my dreams come true basi.. Wema mimi natembelea vimeo lakini siwezi kukubali wewe ushuke huku.. Wema its hight time u stand and this is high time to understand kuwa wewe ni star and u deserve the best from ya fame…!! People loves u so much…..
Read more >>

JWTZ MILIONEA ALIVYOUAWA KWA RISASI, SOMA ZAIDI HAPA

NI taharuki iliyojaa majonzi na simanzi kufuatia Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU jijini Dar kuondokewa na mpiganaji wake, Sajenti Yohana  Lugendo Gweso (40) ambaye alikuwa milionea aliyepigwa risasi sita mwilini na kufariki dunia papo hapo.
Mwili wa marehemu Sajenti Yohana Lugendo Gweso (40) wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ Kikosi cha CMTU ukiwa kwenye jeneza.
Tukio hilo la kusikitisha, lilijiri saa 1:45 usiku wa Septemba 22, mwaka huu, Ukonga Babana ndani ya baa maarufu ijulikanayo kwa jina la Super Karatu.
UWAZI HATUA KWA HATUA
Kufuatia tukio hilo, Uwazi kama kawaida yake lilifuatilia kwa kina ili kubaini yaliyofichika nyuma ya pazia kama siyo sirini!
Gari kubwa la jeshi lililoandaliwa kwa ajili ya kuuchukua mwili wa marehemu Sajenti Yohana  Lugendo Gweso kwenda Bunda kwa mazishi.
Habari zilizopatikana zilidai kuwa, siku ya tukio, marehemu Gweso alipigiwa simu akiwa njiani kurudi nyumbani kwake akitokea Hospitali ya Dar Group iliyoko Tazara jijini Dar.
Ikadaiwa kuwa, baada ya kupata simu hiyo alifika kwanza nyumbani kwake Gongo la Mboto kambini.
“Alipofika alikula chakula cha mchana kisha alipumzika. Ilipofika saa 11 jioni aliondoka kwenda kwenye shughuli zake za biashara. “Alipokuwa huko inadaiwa alipigiwa simu na mtu huyo wa mwanzo na kupanga sehemu ya kukutania ambapo ilikuwa  ni hapo baa,” alisema ndugu mmoja akiomba kusitiriwa jina lake.
Wanajeshi wa JWTZ wakiupandisha mwili wa Sajenti Yohana Lugendo Gweso kwenye gari.
AONDOKA NA NDUGU
Mpiganaji huyo inadaiwa wakati anatoka katika biashara zake alikuwa na mtoto wa dada yake aliyetajwa kwa jina moja la Frank ambaye alikuwa akisimamia hesebu zote za biashara. Siku hiyo walikuwa wamekusanya kiasi cha shilingi milioni 42.

Ikadaiwa kuwa, walipofika Banana kabla ya kuingia Baa ya Super Karatu, marehemu ambaye alikuwa akiendesha gari lake aina ya Toyota Prado lenye namba za usajili T 855 BWK, alimshusha Frank na kumtaka atangulie  nyumbani kwani alihitaji kwenda Super Karatu kukutana na mwanamke huyo ambaye baadhi ya watu wanadai ni mweupe, mnene aliyepanda hewani (mrefu).
Mjane (mwenye kilemba cheupe) wa marehemu Sajenti Yohana  Lugendo Gweso akisaidiwa na ndugu wa karibu kuingia kwenye gari lililoandaliwa kwa ajili ya safari.
AFIKA ENEO LA MAUAJI YAKE
Habari zaidi zinasema kuwa, marehemu aliwasili kwenye baa hiyo saa 1 usiku na kutafuta  maegesho. Alishuka na kuanza kutembea, lakini ghafla kwa  nyuma aliitwa na watu wawili ambao walimuita; “Gweso tuko hapa.”

Wakati anageuka kuwafuata watu hao, watu wengine walianza kuvunja gari lake vioo hivyo alirudi mbio ili kujua nini kinaendelea.
“Kumbe wau hao walikuwa kundi moja na mashambulizi ya risasi yalianzia hapo.
“Marehemu alimiminiwa risasi sita mwilini, alipigwa kichwani, nyingine kifuani na walimchukulia fedha zote milioni 42 na bastola yake kisha wakatokomea,” aliendelea kusema ndugu huyo.
Waombolezaji wakiingia kwenye gari kuelekea kwenye mazishi, Bunda.
MWILI WAKUTWA CHINI
Baada ya tuko hilo ndugu, jamaa na marafiki walijulishwa kuhusiana na kifo cha mjeshi huyo ambapo walifika na kuuchukua  mwili wa marehemu hadi Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar kwa ajili ya kuuhifadhi.

UTAJIRI WA MAREHEMU
Mpaka kifo chake, marehemu Gweso alikuwa akimiliki magari manne ya kisasa, Toyota Prado (alikuwa nalo siku ya tukio), Toyota Verossa, Suzuki Vitara na VRS.
Aidha, alikuwa akimiliki biashara mbalimbali kama vile baa, duka la bia za jumla na nyumba ya kulala wageni. Vyote vipo Ukonga, Dar.
Waombolezaji wakiuchukua mwili wa Sajenti Yohana  Lugendo Gweso kwa ajili ya mazishi.
Baadhi ya waombolezaji siku ya msiba walimtaja marehemu kuwa mwanajeshi milionea aliyehakikisha anapiga hatua kwa biashara kila kukicha.
ALIANZA KUWINDWA MWAKA 2008
Habari zaidi zinadai kuwa, marehemu alianza kuwindwa mwaka 2008 ambapo watu wasiojulikana majina, sura wala nia yao, walivamia nyumbani kwake, Banana (uswahilini) na kumpiga risasi mtoto wa dada yake na kufariki dunia papo hapo.
Sajenti Yohana  Lugendo Gweso enzi za uhai wake.
Inadaiwa watu hao waliamini mtoto huyo ni Gweso mwenyewe lakni yeye hakuwepo. Kufuatia tukio hilo, marehemu aliomba kuhamia kambini kwa usalama wake hadi kifo kilipomkuta hivi karibuni.
MAZISHI YAKE
Marehemu Gweso amezikwa Septemba 27,  mwaka huu katika Makaburi ya Kijiji cha Tailo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara. Ameacha mke mmoja na watoto wanne
Read more >>

USHIRIKINA: PAKA AFUNGWA HIRIZI NYEUSI MTINI

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa hai alikutwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo mkoani hapa.
Paka mwenye hirizi kubwa shingoni akiwa amepigiliwa misumari juu ya mti uliopo jirani na Msikiti wa kwa Mtawara uliopo Kata ya Mwembesongo, Morogoro.
Tukio hilo lililokusanya umati mkubwa wakiwemo waumini wa msikiti huo lilitokea alfajiri ya Alhamisi iliyopita ambapo baadhi ya waumini wa msikiti huo walikuwa wamefika msikitini kwa Swala ya Alfajiri.
Baadhi ya waumini wa msikiti huo walipohojiwa na mwandishi wetu walisema alfajiri hiyo walisikia sauti ya paka akilia kutoka kwenye mti huo uliopo kandokando ya Barabara ya Mtawara inayoelekea Kichangani na Mji Mpya.
Watoto wakishudia tukio hilo la kushangaza.
“Tulifika hapa msikitini kwa lengo la kuswali Swala ya Alfajiri kwa kuwa bado kulikuwa na giza hatukuweza kumwona, lakini tulisikia akilia kwa kupiga kelele mfululizo.
“Tuliposogelea tulimwona akiwa juu ya mti huku amevishwa hirizi kubwa ya rangi nyeusi. Haya ni mambo ya kishirikina, tena tuna wasiwasi hata wa maisha yetu.

“Unajua eneo hili lina miti mingi lakini wahusika wamekuja kumpigilia misumari paka huyu hapa. Mimi nasema wasakwe hawa watu tuwajue,” alisema muumini mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Abdallah Said.
Umati wa watu wakishudia tukio hilo linalohusishwa na ushirkina.
Naye mjumbe wa kamati ya utendaji ya msikiti huo, Haji Said Dihole alipohojiwa na mwanahabari wetu alisema:
”Kama kuna mtu alitaka kutujaribu angemuweka paka huyo kwenye eneo letu la msikiti angeipata habari yake, pia nasikia tukio kama hili liko kwa majirani wetu pale Kanisa la T.A.G Mwembesongo, nenda kashuhudie.”

Paka huyo baada ya kutolewa mtini.
Baaada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alifunga safari hadi kwenye Kanisa la Tanzania Assemblies of  God ‘T.A.G’ linalofahamika kwa jina la Bethel Revival Temple lililopo Mwembesongo.
Mwandishi wetu hakumkuta paka lakini wananchi wa eneo hilo walipoulizwa walikiri kuwepo kwa paka huyo kwenye mtaa huo lililopo kanisa hilo lakini aliondolewa.

Baadhi ya wananchi wakimwangalia paka huyo kwa karibu zaidi.
Haikufahamika mara moja mtu aliyeamua kuweka paka hao kwenye maeneo ya jirani na nyumba za ibada alikuwa na malengo gani.
Read more >>

FUNDI SEREMALA AJINYONGA NA KUACHA MASWALI

KATIKA hali ya kushangaza, mtu mmoja ambaye ni fundi seremala aitwaye Emmanuel Carlos, mkazi wa Kwabinyau Magomeni jijini Dar amekutwa akiwa amejinyonga saa mbili asubuhi Septemba 23, mwaka huu katika kile kinachodaiwa kuchoshwa na mgogoro wa kifamilia.
Emmanuel Carlos enzi za uhai wake.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, kwa muda mrefu, marehemu alikuwa na mgogoro usioisha na mkewe Mariamu Suleimani uliosababisha wawili hao kulala katika vyumba tofauti ndani ya nyumba yao.
Baadhi ya majirani wa eneo hilo walisema kutokana na ugomvi huo, marehemu alikuwa akirudi nyumbani usiku akiwa amelewa na kumtukana matusi mkewe huku baadhi wakienda mbali na kudai alikuwa haachi hela ya matumizi.
Hata hivyo, mkewe marehemu anadaiwa kuwa na biashara yake ya samaki na alikuwa akijituma ili kuhakikisha anapata nauli ili arejee nyumbani kwao.
Mke wa marehehu akilia kwa uzuni.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyopatikana, mtu wa kwanza kujua kuhusu suala hilo alikuwa ni kijana wake mwenye umri wa miaka saba, Celestine Carlos aliyekwenda chumbani kwa baba yake kuomba hela ya shule, ambapo alimkuta akining’inia kwenye dari baada ya kuwa amejifunga kamba kwenye feni.
Akizungumza na waandishi wetu Mariamu alisema kuwa siku moja kabla ya tukio, mumewe alirudi nyumbani na kumtukana huku akilia na kumwambia kuwa atamkumbuka sana katika maisha yake na kwamba kabla ya kupambazuka mmoja wao atakuwa amekufa.
“Siku iliyofuata alipoamka alinikuta naosha vyombo, akanitazama kwa jicho baya kisha akaenda chumbani kwake ambako alijifungia.
Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la tukio.
Nusu saa baadaye alikuja mwanaye Celestine na kuniomba hela ya shule, nikamwambia aende akachukue kwa baba yake, alipoingia akarudi na kuniambia baba yake ananing’inia, jambo nililoona kama utani lakini baadaye nilienda na kumkuta akiwa amejinyonga,” alisema Mariamu huku akilia kwa uchungu.
Naye mjumbe wa serikali ya mtaa huo, Jumanne Mneka alikiri kufahamu mgogoro wa familia hiyo na kusema walikuwa wakiwasuluhisha kila mara.
Polisi wakiwa eneo la tukio.
“Juzi kati tu tumetoka kuwapatanisha, nashangaa leo saa mbili asubuhi napokea taarifa kuwa Emmanuel amejinyonga, nimehuzunika sana,” alisema.
Majirani wakiwa wameshtushwa na kushangazwa na jambo hilo, waliungana na wapita njia kwenda kushuhudia tukio hilo, hali iliyoufanya mtaa huo usipitike kwa muda.
Waandishi wetu waliwashuhudia polisi wakifika eneo hilo na kuuchukua mwili na kuupeleka katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya uchunguzi. Marehemu ameacha mke na watoto wawili.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger