
Kabla ya tukio hilo la Soweto, mtu mmoja asiyejulikana alirusha bomu la mkono katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Mei 5 mwaka huu na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 30.
“Milipuko yote miwili inaelekea kufanana lakini bomu la Olasiti, liligundulika limetengenezwa nchini Urusi na namba zake za usajili hazikupatikana. “Lakini hili la Soweto ni tofauti kidogo, namba zake zimepatikana na imegundulika limetengenezwa China na hivyo wataalamu kutoka China wako hapa kwetu wanaendelea kubaini nani aliuziwa kwa sababu huwa yanatengenezwa kwa kufuata namba,” alisema.
Kwa mujibu wa Mulongo, taarifa za awali za makachero wa Polisi nchini, zimebaini kuwa watu waliohusika na milipuko miwili ya mabomu jijini Arusha, walianzia mipango yao jijini humo.
Mulongo alisema ukweli utadhihirika hivi karibuni na kuwataka wananchi kuwa na subira, ili vyombo husika vikamilishe uchunguzi wake.
Alisema Serikali itamchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali cheo chake, kwani mambo hayo ni ya kudhalilisha na kufedhehesha.
Aliwashukuru wakazi wa Arusha waliofika kutoa ushahidi wa watu waliohusika katika tukio la Soweto, na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea kwa makini, ili kuepuka kukamata watu wasiohusika.
Aliwataka wanasiasa nchini, kutotumia milipuko hiyo ya mabomu kuwa ajenda za kisiasa, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuidhalilisha Tanzania nje ya nchi, na kuipotezea wageni, jambo ambalo linaweza kuipotezea mapato mengi ambayo imekuwa ikiyapata kutokana na utalii
No comments:
Post a Comment