Na Nathaniel Limu, Singida.
MAHAKAMA
kuu kanda ya kati inayoendelea na vikao vyake mjini Singida,imemhukumu
Magreth Omari Mshanangu (52) mkulima mkazi wa kijiji cha Nguvumali
wilaya ya Iramba,adhabu ya kutumikia jela miaka nane baada ya kukiri
kosa la kumuuawa mume wake Daudi Mlangi bila kukusudia.
Pia
mtoto wa mshitakiwa Magreth,Shaban Hassan @ Benjamini (22),naye
amehukumiwa adhabu ya kutumikia jela miaka minane baada ya kukiri kosa
la kumuuawa baba yake wa kambo Daudi Mlangi bila kukusudia.
Mshitakiwa Shaban ni mkazi wa kijiji cha Mlandala kata ya Ndago wilaya ya Iramba mkoa wa Singida.
Awali
washitakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya
kukusudia,lakini mahakama hiyo ilibadilisha kosa na kuwa la kuuawa bila
ya kukusudia.
Mapema
mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Caren Mrango,alidai mbele
ya jaji wa mahakama kuu Cresentia Makuru,kuwa mnamo aprili mbili mwaka
2012 saa saba mchana huko katika kijiji cha Nguvumali wilaya ya
Iramba,washitakiwa kwa pamoja walimnyonga hadi kufa Daudi Mlangi.
Amesema kuwa wanandoa hao ndoa yao ilikuwa ilikuwa imetawaliwa na misuguano na ugomvi wa mara kwa mara.
Mrango
amesema siku ya kutukio,marehemu Mlangi alirejea nyumbani saa saba
mchana na baada ya muda mfupi,ugomvi ulizuka baina ya wana ndoa hao na
kisha kuanza kupigana.
Amesema
katika ugomvi huo,Magreth aliweza kumng’ata kwa meno mume wake katika
sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni.Wakati huo huo Shaban alikuwa
akijimnyonga baba yake wa kambo shingoni kwa kutumia kamba.
Mwanasheria huyo amesema katika hekaheka hizo,zilisababisha kukatisha maisha ya Daudi Mlangi.
Kabla
ya kutolewa kwa adhabu hiyo,wakili wa kujitegemea Raymond Kimu,aliiomba
mahakama hiyo iwaonee huruma wateja wake kwa vile kosa hilo ni la
kwanza kwanza kwao toka wazaliwe na kwamba hawajaisumbua mahakama kwa
kitendo chao cha kukiri kosa la kuuawa bila kukusudia.
Jaji
Makuru amesema kwa kuzingatia maelezo ya pande zote mbili,mahakama hiyo
imefikia uamuzi wa kutoa hukumu ya adhabu ya kutumikia jela kila mmoja
miaka nane ili iwe fundisho kwao na watu wengine wanaotarajia kutenda
kosa la aina hii.


No comments:
Post a Comment