Akizungumzia hatua ya
vikosi vya JWTZ kupewa jukumu jipya nchini Kongo, Msemaji wa jeshi hilo
nchini, Luteni Kanali Erick Komba alisema kuwa hilo si jukumu jipya bali
ni jukumu la kawaida, ambalo wanalitekeleza kulingana na maagizo ya
Umoja wa Mataifa.
“Kwa wapiganaji wetu hilo sio jukumu jipya,
wanatekeleza majukumu yao ya kawaida, wamekuwa kazini kila siku, hakuna
siku ambayo wamepumzika, jukumu lao ni kuhakikisha vikundi vya waasi
vinakwisha, sasa kila kinapoibuka na kama wanatakiwa kuwashughulikia
wanatekeleza hilo, hakuna jukumu jipya hapo,” alisema Luteni Kanali
Komba.
Kuhusu wanajeshi hao kurejea nchini kuanzia mwezi Aprili,
alisema suala hilo ni la ndani na hawezi kulizungumzia na kwamba wakati
wa kufanya hivyo ukifika atazungumza.
“Ndugu yangu suala la
kurudi ama kutorudi ni la ndani, wale wako kule kwa ajili ya kulinda
amani, wakati wa kulizungumzia hilo ukifika bila shaka tutafanya hivyo,”
alisema.
>>Mtanzania
>>Mtanzania

No comments:
Post a Comment