Linex Sunday Mjeda, ambaye hivi karibuni ameonekana kwenye picha
kadhaa akipoz na video Queen maarufu Tanzania, Agnes Gerald (Masogange),
amekanusha kuwa na uhusiano wa mapenzi na mrembo huyo.
Kupitia akaunti yake ya Facebook, mkali huyo wa ‘Kimugina’ ameonesha
kusikitishwa na habari iliyoandikwa na tovuti moja kuwa yeye na Agnes
wako kwenye mapenzi mazito.
“Ni kweli watu wa blog mnapush sana kazi zetu but nimesikitishwa na
habari hii iliyoandikwa na blog kadhaa mtasababisha tutashindwa ata
kukaa na Dada zetu au marafiki zetu Uliza b4 Hujaandika ujinga am single
na sina haraka ya kua na mpenzi.” Ameandika kwenye Facebook.
Wikendi hii, Linex alipost picha mbili Instagram akiwa na mrembo
huyo, moja wakiwa wamepoz ufukweni, na nyingine akiwa naye katika mechi
ya mpira wa kikapu kati ya timu za madirector wa video za muziki
Tanzania, Adam Juma na Karaban.
>>Times 100.5 FM
>>Times 100.5 FM

No comments:
Post a Comment