Akizungumza na tovuti ya Times FM, boss wa kampuni hiyo, Ostaz Juma
amedai kuwa hatua hiyo imetokana na utovu wa nidhamu uliooneshwa na
msanii huyo kwa kutofuata sharia za Watanashati Entertainment, ikiwa ni
pamoja na kufanya shows bila kuutarifu uongozi.
‘Unajua PNC alipokuja Mtanashati aliniomba nimsimamie kazi zake kwa
kutumia fedha zangu, lakini unakuta anapoenda kupiga show kadhaa
hanijulishi, wakati mimi ninatumia pesa nyingi sana kumgharamikia, sasa
kuna umuhimu gani wa mimi kumsimamia? Ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Sio yeye tu, na Dogo Janja, wote hawana utovu wa nidhamu kabisa,
mara kumi fedha zangu nizipeleke msikitini au kwa watoto yatima
nibarikiwe kuliko kukaa na watu wasiokuwa na nidhamu.” Boss wa
Watanashati ameongeza.
Tovuti ya Times Fm, ilizungumza pia na PNC ambaye licha ya kukiri
kuondolewa Watanashati, alikanusha madai ya Ostaz Juma ya kuwa mtovu wa
nidhamu.

No comments:
Post a Comment