JB akizungumza kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya“Habari nilizozinyaka kutoka kwa chombo cha uhakika ni kuwa wasanii wa bongo movie walilipwa Tsh. Milioni 8 kwa kuhudhuria maadhimisho ya kutimiza miaka 37 na kujiunga na chama cha mapinduzi. Aliyefanya malipo haya ni Nape Nnauye na walipewa cash nina uhakika mh. Rais hakuwa analifahamu hili,” taarifa hiyo imesema.

Wasanii hao ni pamoja na Jacob Stephen, Irene Uwoya, Blandina Chagula,Mboto,Single Mtambalike, Haji Adamu aka Baba Haji, Slim Omar, Wastara na wengine.

Sherehe hizo zilifanyika kwenye uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, ambapo wasanii hao walikabidhiwa kadi za uanachama.

No comments:
Post a Comment