LILE penzi la msanii wa filamu na mtangazaji, Lulu
Mathias na mchezaji mpira wa zamani, Amani limesambaratika baada ya hivi
karibuni mwanaume huyo kuondoka na kilicho chake huku akimwacha
mwanadada huyo ndani ya nyumba peke yake.
Chanzo chetu makini kilisema kuwa, tukio hilo lilitokea hivi karibuni
huko Majohe walipokuwa wakiishi wawili hao ambapo mwanaume huyo aliamua
kuondoka na kurudi nyumbani kwao na kumuacha Aunty Lulu ndani ya nyumba
hiyo waliyokuwa wamepanga.
Baada ya kuzipata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu, akafunguka:
“Ukweli mimi na Amani tumeachana kwani kipigo kimenizidi kila kukicha
isitoshe ndugu zake hawanipendi, nimebaki peke yangu kwenye nyumba
tuliyokuwa tumepanga huku Majohe na yeye ameondoka na vitu vyake vyote,
amerudi kwao.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment