Kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Chilaga Isaack mkazi wa Yombo
Dar es salaam, amejikuta akiiweka ndoa yake katika hali ya hatari baada
ya kuchelewa kurudi nyumbani toka kazini kwa sababu ya foleni kubwa ya
magari barabarani.
Isaack alisema kuwa aliporudi nyumbani majira ya saa 4 usiku nyumbani
alimkuta mchumba wake amekasirika na alianza kumuuliza maswali ambayo
yalimweka kijana huyo kwenye wakati mgumu na wakati huo dada huyo akidai
kurudishwa kwao.
"Unajua huyu mchumba wangu anadhani kwamba mimi nilikuwa na mwanamke
sehemu fulani wakati haiko hivyo bali ni foleni tu barabarani
iliyonifanya nichelewe kurudi", alijitetea Isaack.
Tatizo la foleni jijini Dar linazidi kuwa kubwa na kutengeneza usugu
jambo linalosababisha raia wengi wa Dar kupatwa na matatizo mengi mno.
Tatizo hili la foleni bado utatuzi wake unaonekana kusuasua licha ya
wahusika kuonekana wakikaza msuri na kuahidi kulipatia ufumbuzi bila
mafanikio yoyote.
Baadhi ya barabara za jijini Dar zikiwa zinamsongamano mkubwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment