Mtandao
wa skype ambao umekua ukitumika na watu mbalimbali duniani kama njia ya
kuwasiliana huku kila mmoja akipata nafasi ya kumuona mwenzake wa
upande wa pili kwa njia ya video, umepata kitu kingine kipya
kitachorahisisha mawasiliano zaidi. (Skype Translator)
Unaambiwa
kabla mwaka 2014 haujaisha, Microsoft wana mpango wa kuileta hii huduma
itumike na kila mtu, yani ni application ambayo inaweza kutafsiri lugha
mbalimbali na kuwawezesha watu wanaowasiliana kwa lugha tofauti
kusikilizana papo kwa papo mfano mtu anaeongea Kijerumani akaongea lugha
hiyo lakini wa upande wa pili akawa anamsikia kwa Kiingereza.


Wanasema
hii imekuja kuvunja mipaka ya matumizi ya lugha, sasa itakuwezesha
kuwasiliana na kuelewana na yeyote ulimwenguni kwa sababu inayachukua
uliyozungumza na kuyaweka kwenye lugha uliyochagua, sauti inakua ileile
ya kiume kama wewe ni Mwanaume au ya kike kama wewe ni Mwanamke.
Kitu
kimoja ambacho sijakifahamu ni kama Kiswahili kitafanya kazi ndani
yake, unaweza kutazama hii video hapa chini ili kuipata zai
No comments:
Post a Comment