Watu
Sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni
Ndejela Express lenye namba za usajili T 257 CMP aina ya TATA
likiendeshwa na Dereva wa kike Vailet Mbinda(31) mkazi wa Sokomatola kugongwa kwa nyuma na roli la mizigo kisha kupinduka Kijiji cha Nanyala Kata ya Nanyala wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa tisa alasiri barabara ya Tunduma/Mbeya ambapo roli lenye namba
T 369 AWM aina ya SCANIA likendeshwa na Dereva asiyefahamika likiwa
katika mwendo kasi liligonga basi kwa nyuma kisha magari yote mawili
kupinduka.
Miongoni
mwa waliofariki ni Zainabu Mohammed aliyekuwa kondakta wa basi hilo
linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Sumbawanga kila siku, Padri
Barnaba Lwemba 35 wa Morogoro Emmanuel Philipo 1 wa Sumbawanga Neusta
Jacob Mafuga 27 wa iringa Milika Mbingamno 38
Mwanaume mmoja na Mwanamke mmoja walifariki eneo la tukio na wawili walifariki wakati
wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wakati majeruhi
wanane walikimbizwa Rufaa kutokana na hali zao kuwa mbaya.
Kamanda
wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kwamba chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na juhudi za
kumtafuta Dereva wa roli zinaendelea.
Aidha
amewataka wamiliki wa magari na madereva kuyafanyia matengenezo na
ukaguzi wa mara kwa mara magari yao ili kuepusha ajali zinazoweza
kuepukika.
Muuguzi
Mkuu wa Hospitali Teule ya Wilaya ya MbeyaIfisi, Sikitu Mbilinyi
amewataja majeruhi kuwa ni Dereva amewataja majeruhi kuwa ni Fred,Maiko
Malema(16),Justin Komb(24),Amir Ramadhan(26),Nausi Bakari(28),Jackson
Kambo(19),Anoria Ndezi(13) na Lucy Edson(17).
Mbilinyi
amewataja wengine kuwa ni Groly Paul(27),Moyo Safi(1),Rahma
Peter(3),Mary Kitine(57),Mariam,Karen Naiman,Mecy,Adelina
Malipesa(52),Suzana Athas(35),Adelina Essau(28),Frola Essau(64) na Emmy
Charles(21).
Wengine
waliolazwa ni pamoja na Diana Jumbe(19),Esther Seleman(21),Paul
Mayeta(45)ambaye ni Dereva msaidizi,Bahati Julius(33) na Joeph
Komba(34).
Kwa
mujibu wa Muuguzi Mkuu hali za majeruhi zinaendelea vizuri na wanafanya
kilajitihada za kuokoa maisha yao na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza
kuchangia damu kwani Hospitali hiyo ina uhitaji mkubwa kutokana na kuwa
karibu ya barabara kuu na ajali zinazojitokeza mara kwa mara ingawa
hupatiwa damu kutoka Benki ya Damu salama.
Hata
hivyo baadhi ya abiria wamelalamikia kitendo cha baadhi ya wananchi wa
Nanyala badala ya kusaidia majeruhi walikuwa wakiwapora mizigo,simu na
fedha pia waliokuwa na vito vya thamani kama heleni.
Jackson
Kambo ambaye ni mmoja wa wahudumu wa basi hilo amesema kuwa kama
ushirikanowa wananchi hao wangeutoa mapema kondkta wake aingefariki
lakini badala ya kusaidia walikuwa wanan’gan’gania mkoba wa fedha hadi
walipofanikiwa kuchukua fedha ndipo walianza kutoa msaada marehemu akiwa
amelaliwa mkono na basi.
Kambo
amesema kama si juhudi binafsi Dereva wa basi angepoteza maisha
kutokana na kubanwa na mkanda hivyo kulazimika kuukata na kuanza
kusaidia kuokoa abiria wengine.
|
No comments:
Post a Comment