Baada ya MTV MAMA awards iliyofanyika huko bondeni Afrika ya kusini na
kuteka akili za watu hapa town, haswa baada ya mkali wa Afro Pop kupiga
bonge la show ambalo lilimchanganya hadi Mr.President na kumfanya
afunguke kukubali na show ile...
Hii sasa ni moto wa kuotea mbali, huku wakati Diamond Platnumz
akiwa bado ana-run hii DSM, hasa baada ya kuachia nyimbo yake ya Mdogo
mdogo inayopigwa kila kona ya media hapa Bongo. Hivi sasa ni moja kwa
moja hadi jiji la malaika aka Los Angels huko kwa Obama ambapo ndipo
anatarajia kutia mguu katika maandalizi ya awali ya tuzo hizo za BET.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram alifunguka na kudokezea tu, akisema
“LOS ANGELES! need i say More?”, kweli hamna la ziada la kusema hapo
lugha ya picha hii inasomeka vizuri sana.
No comments:
Post a Comment