DAYNA AFUNGUKA KUHUSU SKENDO YA KIMAPENZI NA MSHIRIKI WA BIG BROTHER.

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dayna aliye-make headlines na kuzidi ku-hit kwenye tasnia hii ya muziki wa Bongo fleva, hatimaye afunguka kuhusu picha zilizokuwa zinaleta utata kwenye mitandao na Blogs mbalimbali nchini,

huku ikibua maswali mengi kuwa wawili hao ni wapenzi au la.”Habari hizo si za kweli, mimi na Nando ni marafiki tu tulioshibana, na ndio maana tumeweza kupiga picha zenye ukaribu namna hiyo, kama ilivyo kwa marafiki walioshibana yeye mara nyingi hunipa kampani, na mimi pia huwa nampa kampani, ila hakuna mahusiano yoyote ya mapenzi yanayoendelea baina yetu, ni Marafiki tu toka zamani”- alimalizia kufunguka Dayna, kuweka sawa utata wa picha alizoweka kwenye mtandao wa instagram na kuzua utata mkubwa.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger