Ajifungua mtoto mwenye kichwa cha nyani Tukio la aina yake na lakushangaza limetokea huko nchini Nigeria baada ya Mwanamke mmoja mkazi wa Kaduna,ambaye jina lake halikuweza kutambuliwa mara moja ameripotiwa kujifungua mtoto anayefanana na nyani kwa sura, masikio na macho.
Kwa
mujibu wa vyombo vya habari vya nchini Nigeria, tabibu aliyemhudumia
mwanamke huyo katika hospitali ya serikali amesimulia tukio hilo
lilivyokuwa.
“Alikuja
mwanamke mjamzito majira ya saa moja na nusu asubuhi, Jumapili na
tukamkimbiza chumba cha wazazi.” Amesema wakati wanamhudumia waliona
dalili za kujifungua lakini hazikuwa za kawaida.
“Alikuwa
akitokwa damu mfululizo, nikaagiza aje daktari wa wanawake ambaye
alimpeleka chumba cha upasuaji kwa lengo la kumfanyia upasuaji. Wakati
tunajiandaa, mtoto akaanza alianza akitanguliza miguu. Kwa hiyo daktari
akaniambia tuache ajifungue mwenyewe.”
Amesimulia
kuwa waliendelea kuyashuhudia maajabu hayo na mwisho wakabaki midomo
wazi pale walipomuona mtoto akiwa nusu binadamu nusu nyani na kwamba
alifariki muda mfupi baadae.
Amesema
mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo nne na kwamba mama yake
anaendelea na matibabu kwa kuwa alitokwa damu nyingi sana wakati
anajifungua.
No comments:
Post a Comment