MASTAA wa kike wanaotingisha Bongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ (pichani) na Husna Maulid, ilibaki kidogo wazichape,
Amani lina mchapo mzima.
Kabla ya tukio hilo, awali wawili hao waliwahi kuingia kwenye bifu
baada ya kudaiwa walikuwa wanamgombea pedeshee mmoja wa mjini, kila
mmoja akijipa uhalali wa kumilikiwa.
Tukio hilo bichi kabisa
lilitokea Juni 16, mwaka huu, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo
chanzo kinasema, wadada hao walikuwa wakirekodi sinema ambayo
haijajulikana jina lake.
“Ni kweli walikuwa wakirekodi filamu, lakini kuna muda walizinguana
ila watu wanasema bado wanakasirikiana kutokana na ile ishu ya
kunyang’anyana mwanaume.
“Joti (Lucas Mhuvile – yule komediani wa Kundi la Orijino Komedi)
alikuwepo eneo la tukio na ndiye aliyewapatanisha,” kilipasha chanzo
hicho.
Joti alipotakiwa kuzungumzia ishu hiyo, alikiri kutokea lakini kwenye kurekodi filamu huku akikataa kufafanua.
“We’ jua kuwa ilikuwa filamu, si ugomvi serious,” alisema Joti.
Lulu hakupatikana kuzungumzia ishu hiyo lakini Husna alipopatikana
alisema: “Tulitofautiana kikawaida tu kama wanawake lakini hatukufika
kwenye mambo ya kupigana.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment