SAJENTI: SIWEZI KUMSAHAU CHAZ BABA KWA KITENDO CHA KUMKANA MWANANGU

MIMI napenda kukuuliza kwa nini uliachana na mwanamuziki Chaz Baba na inavyoonekana mnaendana sana? Selemani Alifa, Dar, 0718803204
SAJENTI: Kila kitu kina wakati wake hivyo ule ulikuwa ni wakati wangu lakini haikuwa riziki.

Mwanamuziki Chaz Baba.
PICHA ZA UTUPU
Kwa nini unapenda kupiga picha za utupu? Huoni kama unaishusha hadhi yako? Andrew Kazala, Dar, 0717179570
SAJENTI: Sijawahi kupiga picha za utupu.

URAFIKI
Sajenti kiukweli wewe ni msanii mahiri kunako kiwanda cha filamu Bongo, naomba uwe shosti wangu wa kubadilishana mawazo. Salim Liundi, Dar, 0659601205
SAJENTI: Asante, karibu sana.

ANATAKA AMUOE
Napenda sana utulivu wako Husna, vipi umeolewa? Kama bado naomba nafasi. Muddy Madiley, 0652672805
SAJENTI: Sijaolewa nina rafiki wa kiume.

VIPI KUHUSU IDD?
Nimeshawahi kukuona mtaani kwetu na jamaa mmoja anaitwa Idd ulikaa naye kama wiki hivi, vipi ndiye shemeji? Shadee Sharif, Dar, 0713815145
SAJENTI: Umenifananisha siyo mimi.

Muigizaji wa sinema Bongo, Husna Idd, 'Sajenti'.
CHANGAMOTO
Dada Husna nataka kujua changamoto ulizozipata wakati unaanza sanaa ya uigizaji hadi kufikia kuwa staa hususan wewe ni msichana mdogo. Pia una mpango gani kuhusu kuwasaidia kina dada wenzako wenye vipaji lakini hawajapata sapoti yoyote?
Florah Malya, Dar, 0717797938

SAJENTI: Changamoto nimekutana nazo za kawaida tu kama msichana  kuhusu kuwasaidia wenzangu kwa sasa bado kwa sababu mimi mwenyewe nahitaji msaada.
ANAJIEPUSHAJE NA SKENDO
Vipi unajiepushaje na skendo kama wasanii wengine wanavyokuwa na skendo? Msomaji, 0652891958
SAJENTI: Ninajiheshimu tu hakuna la zaidi.

WEWE NI MWENYEJI WA WAPI?
Sajenti wewe ni mwenyeji wa mkoa gani? Hawa Alfan, Dar, 0713455487
SAJENTI: Mimi ni mwenyeji wa Dodoma.

VIPI KUHUSU UBORA WA FILAMU?
Filamu kwa sasa zinatazamwa na wengi, je, ninyi kama wasanii mnafanya nini ili kuwapa watu vitu bora? Elia, Iringa, 0718085308
SAJENTI: Kikubwa tunaangalia stori nzuri zenye ujumbe kwa jamii.

YEYE NA KABULA WANA BIFU?
Dada naikubali sana kazi yako lakini je, ni kweli una bifu na Jini Kabula? Halafu naomba uwe rafiki yangu. Jackson Benard, Dar, 0714680634
SAJENTI: Jini Kabula ni rafiki yangu wa muda mrefu sana na hatujawahi kugombana, kuhusu urafiki karibu sana.

HISTORIA
Dada Sajenti naomba historia yako kwa ufupi umesoma hadi wapi, umri, kabila, una familia na tofauti na sanaa unafanya kazi gani? Msomaji, 0719125145
SAJENTI: Nina elimu ya kidato cha nne, sijaolewa ila nina mtoto mmoja anayeitwa Carina tofauti na sanaa ninafanya biashara ya nguo.

KITU AMBACHO HATAKISAHAU
Hongera kwa kazi, je, ni tukio gani ambalo huwezi kulisahau hadi leo? Jose, 0757904855
SAJENTI: Sitasahau siku ambayo Chaz Baba alimkana mwanangu na kusema kwamba siyo mtoto wake.

AMEJIFUNZA NINI KWENYE MAPENZI?
Dada Husna katika kuishi kwako kote umejifunza nini juu ya mapenzi halafu kwa nini wasanii wa kike hamuolewi? Rich Boy, Tabora, 0783093909
SAJENTI: Nimejifunza kutomwamini sana mwanaume, kuhusu kutoolewa siyo kweli mbona mastaa wengi wameolewa? Tuliobaki bado riziki yetu haijafika, ikifika tutaolewa tu.

ANA MPANGO WA KUIGIZA UCHI?
Dada Sajenti mimi nakukubali sana ila nilipata habari kuwa unataka kwenda kuigiza nusu uchi nje ya nchi, kuna ukweli wowote? Msomaji, 0718173696
SAJENTI: Sijawahi kuongelea hivyo vitu na sitajaribu.

FILAMU ALIZOCHEZA
Nakukubali sana Sajenti ila sijawahi kuona filamu yako hata moja, je, unaweza kunitajia baadhi nizifuatilie? Sophia, Dar, 0769607091
SAJENTI: Nimecheza nyingi kama Same Girl,  Scholar, Sobbing Sound, Men’s Day Out na nyingine kibao.
KUHUSU TATOO YA CHAZ BABA?
Husna ni kweli ulijichora tatoo ya sura ya Chaz Baba kwenye sehemu za siri? Advera Maunda, Dar, 0712515179

SAJENTI: Siyo kweli.
UGOMVI WA KILA SIKU VIPI?
Wewe kama kioo cha jamii unazungumziaje ugomvi wa kila siku wa masupastaa? Tedy, Morogoro, 0759785305

SAJENTI: Sina cha kuzungumzia ila sipendi wanavyogombana kwa sababu wao ni kioo cha jamii hivyo jamii itajifunza nini kwao? Siyo vizuri.
HUYU ANATOA POLE
Poleni sana kwa misiba mfululizo sasa huu ni wakati wa kumrudia Mungu kuna kitu anawakumbusha.  Msomaji, 0686596140

SAJENTI: Asante.
ANA MALENGO GANI?
Vipi dada una malengo gani mpaka sasa katika usanii wako? Maria Boaz, Tunduma, 0766941609
SAJENTI: Nina malengo ya kuwa staa wa kimataifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger