
Mapenzi yaliyopitiliza ya shabiki wa muziki
wa Marehemu Whitney Houston yamemfanya kununua nyumba ya mwanamuziki
huyo na kuahidi kuitunza kwa ajili yake.
Nyumba hiyo ya Whitney iliyopo katika mji wa
Mendham huko New Jersey imeuzwa kwa takribani dola milioni 1.5 kwa
Matthew Krauthamer, ambaye ni shabiki wake na amedai kuwa hataki
kuibadilisha nyumba hiyo yenye ukubwa wa hekari tano.

Wakati mwanamuziki huyo ananunua nyumba hiyo aliiongezea studio ya kurekodi muziki, chumba cha michezo, chumba cha burudani, uwanja wa mchezo wa Tennis na nyumba ya bwawa la kuogelea na mmiliki huyo mpya amesema anataka kuifanya nyumba hiyo ya kiburudani zaidi.
No comments:
Post a Comment