WASANII NCHINI KUTUNUKIWA TUZO KUTOKANA NA KAZI ZAO

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mungereza (wapili kushoto) akiserebuka na wasanii wa Kundi la Jipe Moyo la mkoani Dodoma.
Waalikwa wakifuatilia mambo.
Waziri Mukangara akicharaza gitaa la solo.
Mwanamitindo maarufu nchini, Asia Haidarus akimzawadia Waziri Mukangara vazi alilobuni.
Burudani zikiendelea.
Sanaa ya uchoraji pia ilikuwepo, waziri alikabidhiwa picha iliyochorwa papo hapo.
Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Dokta Fenella Mukangara jana usiku alizindua maadhimisho ya Siku ya Msanii hapa nchini ambayo huadhimishwa Oktoba 25 kila mwaka ulimwenguni kote. Maadhimisho hayo yalifanyika kwenye Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Masaki, Jijini Dar es Salaam.
Waziri huyo alisema kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar, ambapo wasanii wa fani mbalimbali wakiwemo wanamuziki, wachoraji na wengineo watatunukiwa tuzo. Dokta Mukangara pia amesema serikali kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa 'Basata' ndiyo waratibu wa maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger