SIKU
chache baada ya kukutwa mauzauza katika kaburi la mwigizaji Rachel
Haule ‘Recho’, kaburi la mwigizaji Adam Kuambiana (pichani)limekutwa
limetoboka kimaajabu.
Gazeti
la Risasi Jumamosi toleo la Julai 19, mwaka huu lilikuwa na babari
yenye kichwa cha habari kisemacho: ‘Uchawi kaburini kwa Recho.
Kwenye
habari hiyo, ilielezwa kuwa katika kaburi la Recho kulikutwa tunguri
iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku,
yai moja na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini.
Baada
ya habari hiyo, siku mbili baadaye, chanzo kingine kiliwapigia simu
waandishi wetu na kuwaeleza kuwa mbali na tukio la Recho, kaburi la
Kuambiana limetoboka kimaajabu na kuzua mtafaruku miongoni mwa watu
walioshuhudia kwa mara ya kwanza tukio hilo.
“Jamani
haya ni mambo ya kishirikina, huwezi amini kaburi hili limetoboka
ghafla kimaajabu maana juzi tu nilikuja kutembelea makaburi haya,
lilikuwa halijatoboka,” kilisema chanzo hicho.
Mapaparazi
wetu walifika katika makaburi hayo na kujionea kaburi hilo likiwa
limetoboka huku watu wengi waliokuwepo eneo hilo walidai kuwa tukio hilo
si la kawaida kwani limetokea wakati ambao mvua hazijanyesha.
Walisema
kama tukio hilo lingetokea wakati ambao mvua zinanyesha basi
wasingekuwa na mashaka lakini kwa jinsi ambavyo limetoboka wakati wa jua
kali ni dhahiri kutakuwa na ‘mkono wa mtu’.
“Hapa
bwana tusidanganyane kuna mkono wa mtu, haiwezekani kaburi lisitoboke
kipindi kile cha mwanzo mwanzo lije kutoboka sasa wakati kuna jua kali
namna hii, lazima kuna mkono wa mtu tu,” alisema shuhuda mmoja.
Wengine
walikwenda mbali zaidi kwa kuhoji kulikoni matukio hayo yawe kwa mastaa
pekee na si kwa watu wengine?“Hii si bure hapa wachawi watakuwa na
shida yao binafsi, haiwezekani iwe kwa mastaa tu ndiyo kunakuwa na
mauzauza,” alisikika shuhuda mwingine.
Alipoulizwa
mmoja wa walinzi wa eneo hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe
gazetini, alisema hata yeye hajui kwa nini inatokea katika makaburi ya
mastaa.“Mimi hata sijui kwa nini lakini yamefululiza, juzi tumeona kwa
Recho na leo kwa Kuambiana, tumuombe sana Mungu atuepushe na mabaya,”
alisema mlinzi huyo.
Hata
hivyo, licha ya watu wengi walioshuhudia kaburi hilo kuamini katika
uchawi, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye alionekana ni mcha Mungu
alisema hakuna uchawi wowote zaidi ya ardhi kutitia na kusababisha
mmomonyoko wa udongo.
“Jamani
siyo uchawi, hivi vitu vinatokea. Hapa itakuwa wakati wa kuzika,
kulikuwa na uwazi umeachwa hivyo ardhi iliposhuka kuziba uwazi huo ndipo
iliposababisha tobo,” alisema shuhuda huyo mcha Mungu.
Kuambiana
alikutwa na umauti Mei 17, mwaka huu alipokuwa akipelekwa katika
Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar baada ya kuugua ghafla akiwa
hotelini alipokuwa amepanga kwa ajili ya kuandaa filamu.
via>>Amani
No comments:
Post a Comment