MWIGIZAJI nguli katika
tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel (pichani) anadaiwa kuanza kusaka
mtoto ikiwa ni miaka miwili tangu afunge ndoa na Sunday Dimonte.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Aunt, siku si nyingi staa huyo
atakwenda kuweka makazi ya muda kwa mumewe Dubai hadi atakapopata
ujauzito.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, rafiki huyo ambaye aliomba jina
lake lihifadhiwe kwa kuogopa kusutwa na ‘matarumbeta’, alisema wengi
wanadai mume wa Aunt yuko jela kwa hiyo ili kuwahakikishia kuwa kitu
hicho hakipo ameamua aende kuishi Dubai kwa muda hadi atakaponasa
ujauzito.
“Kama mipango yake itakwenda vizuri, baada ya Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani kupita ataondoka na safari hii atakaa sana Dubai hadi Mungu
atakapomjalia kupata mimba ndipo atarejea Bongo. Lakini baadaye
ataondoka tena kwani hata kujifungua amependa akajifungulie Dubai,”
alisema rafiki huyo.
Baada ya kupata nyepesinyepesi hizo, Amani
lilimtafuta Aunt na kufanikiwa kukutana naye uso kwa uso alipoulizwa
alisema hapendi kuweka hadharani mambo yake na mumewe lakini kuhusiana
na ishu ya kwenda kuishi Dubai, muda si mrefu ataondoka.
“Nadhani unajua kuwa mke na mume Mungu akiwajalia afya njema ni
muhimu ndoa ijibu kwa kupata mtoto, sasa kuhusu kwenda kuishi Dubai
ndiyo mipango yangu.
“Nataka kuwakomesha wale wanaodai kuwa mume
wangu amefungwa! Sitaki kuwajibu kwa maneno, nataka kuwajibu kwa
vitendo,” alitamba Aunt.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment