STAA wa sinema za Kibongo, Haji Adam ‘Baba Haji’
amewatupia dongo kiaina viongozi waliopita kwenye Klabu ya Bongo Movie
Unity kwa kuusifia uongozi wa sasa wa klabu hiyo unaoongozwa na Steven
Mengere ‘Steve Nyerere’.
Akipiga stori mbili tatu na mwandishi wetu, Baba Haji alisema kuwa
uongozi wa Steve umeleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya filamu
Bongo kwa kuwa wamekuwa na umoja na ushirikiano katika masuala ya
kijamii tofauti na uongozi uliopita.
“Nafurahi kuwa na kiongozi mwenye kujali maendeleo na kuwa na msimamo
ambao umetufikisha mbali na kutufanya tuwe na ushirikiano kwenye
matatizo mbalimbali yanayotupata wana Bongo Movie,” alisema Baba Haji.
Uongozi uliopita wa Bongo Movie Unity ulikuwa chini ya Vincent Kigosi
‘Ray’ ambaye alipokea kijiti hicho kutoka kwa Jacob Steven ‘JB’.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment