Ndege iliyopoteza mawasiliano inafanana na hii pichani juu.
SHIRIKA la ndege la Taifa la Algeria, limesema limepoteza mawasiliano
na moja kati ya ndege zake iliyokuwa ikitoka Burkinafaso kwenda Algiers
kupita Sahara.Mawasiliano yalipotea dakika 50 baada ya ndege hiyo kupaa kutoka mji wa Ouagadougou, Burkinafaso shirika hilo limeeleza.
Ndege namba AH 5017 ilikuwa na abiria 110 na wafanyakazi sita wa ndege hiyo.
Chanzo cha habari kimeliambia Shirika la Habari la Ufaransa kuwa ndege hiyo haikuwa mbali na mpaka wa Algeria wafanyakazi wa ndege hiyo walipoambiwa wabadili uelekeo kwa kuwa mawasiliano yalikuwa hafifu na kuepuka hatari ya kugongana na ndege nyingine katika njia ya Algiers-Bamako.
Mawasiliano yalipotea baada ya kubadilishwa kwa njia.
Ndege namba AH 5017 husafiri kupitia njia ya Ouagadougou-Algiers mara nne kwa wiki, AFP imeripoti.
No comments:
Post a Comment