MKE WA WAZIRI WA ZAMANI WA CCM ADAIWA KUMUUA MFANYAKAZI WAKE WA NDANI, KISA UISLAMU WAKE

Mfanyakazi wa ndani wa mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini Cyril Chami (CCM) aitwaye Mariam Said (16) amefariki dunia mapema alfajiri ya leo ikiaminika kwabmba kifo chake kimesababishwa na kipigo toka kwa mke wa Mbunge huyo.


Sababu kubwa ikielezwa kuwa binti huyo ambaye ni muislamu alikataa kwenda kuhudhuria misa kanisani siku ya jumapili na amekua na tabia ya kupinga kwenda kanisani kila mara tangu aajiriwe na mbunge huyo kwa madai kuwa ni kinyume na imani yake (Uislamu).

Msimamo wa binti huyo ulimpelekea kipigo kikali usiku wa siku hiyo (jumapili) ambapo inadaiwa alivunjika mbavu baada ya mke wa mbunge kumpiga na stuli ubavuni.

Majirani wa mbunge huyo wanasema licha ya binti huyo kuvunjika mbavu hakupewa matibabu yoyote badala yake alifungiwa ndani huku akiendelea kulazimishwa kufanya kazi.

Mbaya zaidi mke wa Mbunge huyo alimnyang'anya simu binti huyo ili asiweze kuwasiliana na familia yake na kuwaeleza yaliyompata. Hata majirani walipomuuliza juu ya hali ya mtoto huyo aliwajibu kwa lugha ya kejeli na kuwaambia hakuna mtu anaweza kumfanya chochote, kwani serikali ni yao. Kutokana na maumivu makali pamoja na kukosa matibabu hatimaye binti huyo amefariki dunia leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger