BAADA ya kuachana na mkewe ambaye ni mtangazaji wa
kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Redio Times, Hadija
Shaibu ‘Dida,’ mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha TV1, Ezden
Jumanne ametaja sifa za mwanamke atakayekuja kumuoa kama akitaka kufanya
hivyo.
Akizungumza na mwandishi wetu nyumbani kwake, Kijitonyama jijini Dar,
Ezden alisema kuwa kutokana na kupitia kipindi kigumu cha kuachana na
aliyekuwa mkewe amedai kuwa hafikirii kuoa kwa sasa lakini kama akija
kuoa tena atamhitaji mwanamke mcha-Mungu, mwenye heshima, asiyemlevi na
atakayejitambua kama ni mke wa mtu.
“Sidhani kama nitaoa hivi karibuni, lakini kama nitaoa tena mwanamke
ninayemtaka ningependa awe mwenye heshima, anayefuata dini, asiyependa
ulevi na atakayejitambua kama mke wa mtu,” alisema Ezden.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment