NGANO NA MAFUTA VYAMFANYA VAI WA UKWELI KUTOKWA MABAKA MWILINI

MSANII wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ amejikuta katika wakati mgumu baada ya kutokwa na mabaka mwili mzima.
Msanii wa filamu Bongo, Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’
Hivi karibuni, paparazi wetu alimnasa Vai wa Ukweli akiwa nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambapo alisema anashukuru Mungu kwani yupo kwenye dozi ya mwezi mzima baada ya kugundulika ana ‘aleji’ hivyo kukatazwa na daktari asile vyakula vyenye ngano na mafuta mengi.
Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa na bwanake.
“Yaani mbona sasa hivi nina nafuu, mwanzoni nilikuwa nimevimba sana, nilienda Hospitali ya Mwananyamala wamenipa dawa naendelea kuzitumia mpaka mwezi uishe. Unajua nimeshindwa hata kufunga mwezi huu wa Ramadhani kutokana na kuumwa,” alisema Vai wa Ukweli.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger