Jopo
la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, limeshindwa kusikiliza rufaa
iliyokatwa na upande wa Jamhuri kupinga hukumu ya Mahakama Kuu
iliyomwachia huru Padri wa Kanisa Katoliki, Sixtus Kimaro aliyekuwa
anakabiliwa na kesi ya kumlawiti mtoto wa miaka 17.
Rufaa
hiyo ilipangwa kusikilizwa hivi karibuni lakini hata hivyo padri huyo
pamoja na wakili wake hawakufika mahakamani. Upande wa Jamhuri una hoja
saba katika rufani hiyo.
Kabla
ya kuachiwa huru baada ya kukata rufaa, Padri Kimaro alihukumiwa
kifungo cha miaka 35 jela na kulipa faini ya Sh milioni mbili kwa mtoto
baada ya kupatikana na hatia.
Kutokana
na kushindwa kwa jopo hilo kusikiliza rufani hiyo wiki iliyopita, kwa
kutotokea mahakamani hapo padri huyo wala wakili wake, jopo limeagiza
upande wa Jamhuri kutoa taarifa ya mwito kuwa anahitajika mahakamani
hapo kupitia vyombo vya habari.
Hatua
ya kuamriwa kutumika vyombo vya habari kunatokana na wakili wa
Serikali, Salum Malick kudai kuwa amepata taarifa kutoka kwa msajili wa
mahakama hiyo kuwa, hati ya mwito wa kumtaka afike mahakamani hapo
ilipelekwa kwa Kanisa Katoliki.
Alidai
kwa mujibu wa taarifa hiyo ya msajili wa mahakama, hati hiyo ilipelekwa
Jimbo Kuu la Dar es Salaam lakini waliambiwa na jimbo hilo kuwa Padri
Kimaro si mwajiriwa wao na wala hawajui alipo.
Jopo
la majaji hao watatu ambao ni Engela Kileo, Steven Bwana na Sauda
Mjasiri, limeamrisha mwito huo umtake afike kusikiliza rufaa yake kwa
tarehe nyingine itakayopangwa na mahakama hiyo.
Akitoa
amri hiyo, Jaji Kileo alisema endapo padri huyo hatafika mahakamani
baada ya matangazo hayo, rufaa hiyo itaendelea kusikilizwa upande mmoja.
Katika
kesi ya msingi, Padri Kimaro alikuwa anakabiliwa na mashitaka matatu;
kumlawiti mtoto wa miaka 17, shambulio la aibu na kumdhalilisha mtoto
huyo.
Ilidaiwa
kuwa usiku wa Mei 18 mwaka 2005 katika eneo la Changanyikeni, Dampo,
Padri Kimaro alikamatwa na askari aliyekuwa doria, akitenda makosa hayo.
Katika
hukumu iliyotolewa Agosti 9, 2006 na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa
mahakama hiyo, Pelagia Khaday, Padri Kimaro alipatikana na hatia
katika makosa yote na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 35 jela na
kulipa fidia ya Sh milioni mbili kwa mtoto aliyeathirika na kitendo
hicho.
Alikata
rufaa Mahakama Kuu iliyosikilizwa na Jaji Robert Makaramba, ambapo
aliachiwa huru baada ya Jaji huyo kudai kuwa hakukuwa na ushahidi wa
kutosha kumtia hatiani.
Hata hivyo upande wa Jamhuri umekata rufaa kupinga uamuzi huo wa kuachiwa huru kwa padri huyo wakiwa na hoja saba ya msingi, ikiwa ni kwamba Jaji aliyesikiliza rufaa hiyo alikosea kisheria na kiusahihi kueleza kuwa hapakuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuhusu walichokuwa wakifanya mjibu rufani (padre) na mtoto huyo eneo la Dampo
No comments:
Post a Comment