RIYAMA WA BONGO MOVIE: UKINITONGOZA MIMI SINA HIYANA DAIMA.


Staa wa filamu Bongo, Riyama Ally STAA wa filamu Bongo, Riyama Ally amesema katika maisha yake hajawahi kumtukana mwanaume pindi anaponitokea hata kama hamuhitaji, anamjibu kwa busara.
 Akipiga stori na paparazi wetu, Riyama alisema yeye yupo tofauti na wasichana wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuwatukana wanaume pindi wanapowasilisha hisia zao za kimapenzi kwa sababu tu hawavutiwi kuwa nao.

“Hata kama mtu akinitongoza na nikawa simuhitaji kamwe siwezi kumtukana wala kumuonyesha dharau , kimaadili sisi sote ni binadamu na kila mtu ana hisia zake na maamuzi yake, namjibu tu kistaarabu kwamba mimi nina mtu wangu, kumjibu mwanaume vibaya Mungu hapendi,” alisema Riyama.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger