Akipiga stori na mwanahabari wetu, Wellu alisema amejifungua mwanaye aliyempa jina la Valempia hivi karibuni japo bado hajafunga ndoa lakini anaamini heshima ya kuwa mama kwake ni kitu cha kujivunia.
“Sijutii kuwa mama, hayo mambo ya ndoa ni mipango ya Mungu. Najivunia kuwa mama na ni heshima kubwa ambayo pia naiona kama nisingekuwa naye, nisingeipata,” alisema Wellu.
Wellu, baada ya kuibuliwa na Global Publishers, alijitosa kwenye Bongo Movies na kufanya vizuri hadi sasa.


No comments:
Post a Comment