KUNA STAA wa sinema za Bongo na Miss Tanzania 2006,
Wema Isaac Sepetu ‘ameingizwa mjini’ na mhariri wa filamu Bongo mwenye
asili ya Kiarabu aliyejulikana kwa jina moja la Chidy kwa kuingia mitini
na shilingi 5,000,000 alizompa ili azihariri filamu zake mbili lakini
kazi haikufanyika.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Tanzania Kituo
Kikuu jijini Dar es Salaam, kilisema ilikuwa mwaka jana (2013) ambapo
Wema alimkabidhi mhariri huyo filamu mbili, Super Star na Vian Unaspect.
MALIPO YAFANYWA, KAZI HAKUNA
Ikazidi kudaiwa kwamba mbali na
filamu hizo, Wema alimlipa jamaa shilingi 2,500,000 ili kuzihariri
(editing) filamu hizo ikiwa ni hatua ya mwisho kabla ya kuingia sokoni.
JAMAA AINGIA MITINI, AMKWEPA WEMA
Habari zikazidi kudai kwamba,
baada ya kuudaka ‘mpunga’ huo jamaa huyo amekuwa akimzungusha Wema
kufanya kazi zake na kumkabidhi ili azipeleke sokoni ndipo wiki
iliyopita mlimbwende huyo akalazimika kwenda kutoa taarifa kwenye Kituo
cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ jijini Dar es Salaam.
GHARAMA ZA FILAMU
Kwa mujibu wa mtoa habari huyo, alimsikia Wema akisema filamu zote
zimemteketezea shilingi milioni 70,000,000 mbali na hizo alizomlipa huyo
mhariri wa filamu ambazo zikiingizwa kwenye gharama nzima inafika
shilingi 75,000,000.
KAMA ZINGEINGIA SOKONI
Habari zaidi
zinasema kwamba kama filamu hizo zingehaririwa mwaka jana na kuingizwa
sokoni, Wema angekunja mkobani kiasi cha shilingi 140,000,000 hivyo
kurudisha gharama za kuandaa (75,000,000) na faida juu (65,000,000).
WEMA ASWAKWA, AKATAE AU AKUBALI
Kufuatia maelelezo hayo kutoka
chanzo chetu, mwishoni mwa wiki iliyopita, Uwazi lilimsaka mrembo huyo
ili afunguke kuhusu kuwepo kwa madai hayo, alipopatikana na kuulizwa
sakata zima hakuwa tayari kupepesa macho, akakiri.
Alisema awali kijana huyo aliyemdhulumu alikuwa mfanyakazi wake
katika kampuni ‘mufilisi’ ya Endless Fame, cha ajabu toka ampatie hiyo
kazi ya kumtengenezea pamoja na kumkabidhi fedha amekuwa akimchenga toka
mwaka jana.
“Mimi nashindwa hata kumuelewa ana dhumuni gani na hizo kazi zangu
maana hapo ana kama shilingi milioni 140 zangu, kwa kuwa kila kazi
nilikuwa nalipwa shilingi milioni 70, nilishafanya makubaliano na
Kampuni za Proin Promotion na Steps kuwapa filamu zangu lakini yeye
ananizungusha, toka kipindi kile sijaende China, nikimuuliza majibu yake
siyaelewi.”
WEMA AMWAGA CHOZI, MTUHUMIWA MBARONI
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Wema aliendelea kulalamika mpaka kufikia hatua ya kumwaga chozi:
“Juzi kati Mtitu alitaka nifanye naye kazi lakini akanikumbushia Filamu
ya Super Star, kwamba hajaiona sokoni mpaka sasa, ndipo nikamuelezea,
akasema hawezi kukubali niipoteze kirahisi, lazima nisimame kidete
kuipata ndiyo nikaenda naye mpaka Kituo cha Polisi Mabatini kufungua
kesi na Chidy akakamatwa siku hiyo hiyo.”
APEWA SIKU SABA
Wema aliendelea kusema: “Polisi walimpa siku saba
ahahakikishe ananikabidhi kazi zangu pamoja na kompyuta moja ambayo
aliichukua ofisini kwangu bila ridhaa ya mimi mwenyewe na akagoma
kuirudisha.”
AFISA WA POLISI
Naye afisa mmoja wa polisi wa kituo hicho ambaye
alizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutoandika jina lake gazetini
alithibitisha Wema kufungua kesi Mabatini na ikapewa jalada Namba
KJN/RB/5850/14 WIZI WA KUAMINIWA 3/7/2014.
“Ukweli ni kwamba zikipita siku saba bila kijana huyo kuleta fedha na
kompyuta ya Wema hapa polisi, tutamsaka na tukimkamata sheria itachukua
mkondo wake,” alisema afisa huyo wa polisi.
UPER STAR, OMOTOLA ALIFIKA
Kama itakumbukwa sawasawa Filamu ya
Super Star ilizinduliwa Juni 24, 2012 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro
jijini Dar na nyota wa muvi za Nollywood (Nigeria), Omotola Jalade
Ekeinde alishiriki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment