WOLPER AVAA KIGAUNI CHA MACHANGUDOA NA KUIBUA MINONG’ONO

Stori: Shakoor Jongo
MH! Kigauni kifupi alichotinga staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe katika hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kimeibua minong’ono watu kuhoji kulikoni akivae hivyo ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe
Tukio hilo lilowastaajabisha wengi lilijiri wikiendi iliyopita katika Mgahawa wa Great Wall uliopo Masaki, Dar ambapo asilimia kubwa ya waalikwa katika hafla hiyo walisema hakikustaili hasa kwenye mwezi huu wa toba.
“Unajua siku zote tunaambiwa sisi Bongo Movie hatuna heshima, siyo kweli, kuna watu wapo kwa ajili ya kutudhalilisha. Angalia Wolper alichovaa,” alisema mwigizaji mmoja ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini. Alipoulizwa Wolper kuhusiana na madai hayo ya udhalilishaji, alijibu:
“Achana nao hao ni wanafiki tu kwani kuna mtu amekatazwa kuvaa kama hivi?”

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger