YULE BIBI ALIYEKUFA NA KUFUFUKA, SASA AFA KWA MARA NYINGINE


MKAZI wa kitongoji cha Temeke kilichopo katika Mtaa wa Nanjoka mjini Tunduru Mkoani Ruvuma, Maimuna Omari (62) aliyeripotiwa kufariki Dunia na kurejea katika Uzima ( Kufufuka) Juni 16 mwaka huu afariki tena.
Tukio hilo ambalo limeonekana kuvuta hisia za watu na kufanya Mamia ya wakazi wa kitongoji na mjini wa Tunduru kwa ujumla kujitokeza kujionea maajabu hayo ya Mwezi mungu baada ya mtu huyo kufa kwa mara ya pili.

Wakizungumzia tukio hilo Watoto wa mama huyo Bi. Fatuma Yusuph na Bw. Seremani Yusuph walisema kuwa safari hii kifo cha mama yao kilichotokea July 9 mwaka huu kimedhibitishwa na Wataalamu kutoka katika Hospitali ya serikali ya Wilaya ya Tunduru alikokuwa amelazwa ikiwa ni tofauti na awali ambapo walitumia wazee maarufu na masheikh katika mtaa huo.

Walisema, baada ya kuthibitishwa kwa kifo cha mama yao, waliwaita Bi. Fatuma Mohammed , Bi. Fatu Mbwana na Bi. Zainabu Siyabu kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa Dini ya Kiislamu unaoelekeza kuwa, baada ya mtu kufariki inapaswa marehemu kuoshwa kwa maji ikiwa ni pamoja na kumkamua tumbo kwa ajili ya kutoa kinyesi tumboni, kitendo ambacho akina mama hao walikifanya bila kikwazo chochote.
Wakizungumzia tukio la kwanza walisema kuwa Juni 16 mwaka huu mama yao huyo alifariki dunia akiwa nyumbani kwake majira ya saa 6.00 za usiku na baadae kurejea katika uzima majira ya Saa 4.30 asubuhi wakati wakiwa katika matarajio ya kwenda kumpumzisha katika nyumba yake ya milele saa 7 za mchana wa siku hiyo.

Walisema kifo hicho kimetokea baada ya Mama yao huyo kuugua kwa muda mrefu hali ambayo iliwakatisha tamaa wanafamilia hao hali ambayo iliwalazimu kumtoa hospitali ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kumrejesha nyumbani kwa matazamio ya Ugonjwa huo kutopona.

Wakizungumzia tukio hilo kwa nyakati tofauti Mtendaji wa Kijiji hicho Bi. Zidaya Halifa na Mjumbe wa mtaa huo Bw. Chimwaga Bakari Chimwaga na kwamba marehemu anatarajiwa kuzikwa majira ya Saa 7 .00 za mchana katika makaburi yaliyopo katika eneo la Shule ya Msingi Umoja mjini hapa.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger