Inafurahisha
kuona kuwa wapo wafanyabiashara wengi maeneo tofauti tofauti Nchini
mwetu na mitaa tofauti tofauti wanaouza juisi ya miwa.
Kimsingi juisi hii ni sukari halisia ambayo haijachakatwa.
Sukari halisia ni nzuri kwa mwili kwani ina virutubisho na madini kwa wingi.
Miwa
ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya
kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.
Kijiko
kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11. Madini halisi na vitamin
zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya
chuma na potassium.
Si
hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa
kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya
maziwa.
Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.
Virutubisho
vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji
kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi.
Pia,
wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina
madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukari yake ni
halisia.
-manyandahealthy
No comments:
Post a Comment