WIKI iliyopita
niliishia kwenye maelezo kuwa secondary dysmenorhea huwakumba akina
mama ambao tayari wameshajifungua mtoto mmoja au zaidi lakini wanapatwa
na maumivu makali wakati wa hedhi jambo ambalo hawakuwa nalo siku za
nyuma.
Wiki
hii namalizia kwa kusema kuwa hali hii huchangiwa na mambo mengi
ikiwemo tatizo la kuwa na uvimbe kwenye mji wa mimba unaoitwa mayoma au
fibroid, kuvimba kwa mji wa mimba pamoja na mirija ya uzazi, tatizo
ambalo huitwa P.I.D yaani pelvic inflamatory desease.
Mwanamke
ambaye amekwisha kujifungua na ana tatizo la maumivu chini ya kitovu na
wakati huohuo anatokwa na uchafu kama maziwa ya mtindi ukeni na kupata
hedhi nzito ambayo ina mabonge mabonge ni vizuri akafanya uamuzi wa
kumuona daktari mapema.
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria nini?
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume, hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa umesonga kuelekea miaka 50 au zaidi.
Maumivu chini ya kitovu kwa wanaume huashiria pia tatizo la tezi dume, hasa kama mwanaume anakwenda haja ndogo mara kwa mara nyakati za usiku na umri ukiwa umesonga kuelekea miaka 50 au zaidi.
Dalili
nyingine ambatano ni kutoa haja ndogo ambayo ina kasi ndogo sana
tofauti na kawaida ikiambatana na maumivu ya kiuno na mgongo.
Kwa
wanaume, maumivu haya ya chini ya kitovu huashiria pia tatizo ambalo
kitaalam hujulikana kwa jina la hernia ambapo waswahili tunaita ngiri.
Mwanaume
anaposikia maumivu haya ya chini ya kitovu yakiambatana na maumivu ya
korodani, korodani moja kupungua na nyingine kukua zaidi au zote mbili
kukua au kupotea ni dalili ya ugonjwa huu ambao huharibu ubora wa
uzalishwaji wa mbegu za kiume, ambazo zinaweza kuzalishwa chache au
ambazo hazina kasi ya kutosha kusafiri kwenye via vya uzazi vya mwanamke
na hivyo mwanaume kupoteza uwezo wake wa kutungisha mimba.
Hitimisho
Vipimo na tiba vinahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula.
Vipimo na tiba vinahitajika mapema bila kuchelewa ili kuepuka madhara makubwa katika mfumo wa uzazi, mkojo na hata wa chakula.
No comments:
Post a Comment