Wadada
hao waliyasema hayo, juzi Jumatano baada ya kunaswa na paparazi wetu
maeneo ya Sinza Afrikasana pembeni ya Corner Bar ikiwa ni siku chache
baada ya baadhi yao kukamatwa na polisi ambapo walisema biashara hiyo
ndiyo maisha yao.
Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo.
Walisema, hawapendi kuifanya lakini wanalazimika kutokana na maisha duni waliyonayo.
“Nani
asiyependa kulala usiku na familia yake? Ukituona barabarani ujue hali
ni mbaya. Hata kama polisi wanatukamata lakini wanatuachia na tunarudi
sokoni kama kawaida,” alisema changu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la
Zuena na kuongeza:
“Wateja wetu wenyewe wanajua kuwa hii nguvu ya polisi ni ya soda tu, wakiona tumepigwa ambushi kidogo wanasubiri zipite siku chache kisha tunaendeleza harakati zetu, sisi bila kuja kujiuza hatuwezi kuwasomesha watoto wetu wala kuwalisha.”

Katika
hali ya kushangaza wakati changudoa huyo akizungumza hayo, wapo
waliokuwa wakimshawishi paparazi wetu anunue ngono kwa maelezo kuwa,
hali ni mbaya kwani polisi wamekuwa wakifanya doria mara kwa mara.
“Sasa, achana na mambo ya kutuhoji bwana, tutoe basi kama vipi tukuuzie mambo kwa bei ya ofa. Cheki nilivyojaaliwa,” alisema binti mmoja ambaye ukikutana naye mchana unaweza kusema, ‘mke si ndiyo huyu’.

Hata
hivyo, katika pitapita ya mwandishi wetu maeneo mengi kama vile
Kinondoni, Sinza Mapambano, Mwenge Bamaga na Buguruni, madadapoa hao
wameonekana wakiendelea kujiuza kwa kuibia huku wakiwa makini na kila
mteja anayewatokea.
Aidha,
gazeti hili linalipongeza Jeshi la Polisi jijini Dar kwa operesheni
ambazo limekuwa likizifanya kwani kwa namna moja ama nyingine kasi ya
biashara hiyo imepungua licha ya kwamba wanatakiwa kuongeza nguvu zaidi.
Pia taasisi za ustawi wa jamii na serikali kwa jumla zinatakiwa
kuangalia mbinu mbadala za kuweza kuwaondoa akinadada hao kwenye
mazingira hayo hatarishi.
No comments:
Post a Comment