Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa baa hiyo maarufu iitwayo The
Don, ukumbi wake ambao ulikuwa ukitumika kwa watu kupiga ulabu, hivi
sasa unatumiwa na waumini wa kanisa linalojukana kama Impact
International Christian Centre kupata mahubiri.
Lakini
cha kushangaza ilibainika kwamba katika maandishi makubwa yanayolinadi
jina la baa hiyo, chini yake ndipo limewekwa bango linaloonyesha kanisa
hilo, kitu ambacho kwa mtu mgeni, ni vigumu kuelewa mara moja.
“Siyo baa
hiyo kaka, hilo ni kanisa siku hizi, tumeshangaa ghafla tu waumini
wanakuja na mhubiri wao na wanaendelea na sala kama kawaida. Hatujui
kama huyu mhubiri ndiye alikuwa mmiliki wa hii baa au imekuwaje,”
alisema jirani mmoja wa eneo hilo, aliyekataa kutaja jina.
Hata
hivyo, juhudi za gazeti hili kuzungumza na uongozi wa baa au kanisa hilo
ziligonga mwamba baada ya kuambiwa na majirani kuwa ni nadra kuwakuta
mahali hapo hivyo jitihada zinaendelea.
Katika
miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la kuibuka kwa makanisa
ya madhehebu mbalimbali, ambayo kila moja huwa na watumishi wao
wanaopewa majina kama Mchungaji, Nabii, Askofu na kadhalika.
No comments:
Post a Comment