VIATU VIREFU VYAMUUMBUA MAIMATHA WA JESSE, ATEGUKA MGUU

Na Gladness Mallya
MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse amejikuta akiteguka mguu baada ya kudondoshwa na viatu virefu alivyokuwa amevaa

Paparazi wetu alimshuhudia Maimartha akiwa anachechemea kwenye sherehe moja ya kitchen party hivi karibuni huku akiwa bado amevaa viatu virefu na alipoulizwa kulikoni anachechemea alijibu kwamba aliteguka mguu baada ya kudondoshwa na viatu virefu.

“Nimeumia mguu baada ya kudondoshwa na hivi viatu virefu lakini sikomi kwa sababu navipenda sana na nikivaa ndiyo nakuwa mrembo zaidi,” alisema Maimartha.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger