Hii imetokea Jumamosi pale walipoyatoa matokeo ya wanafunzi waliomaliza mwaka wa nne, na kuwazuilia matokeo yao. Wanafunzi takriban 200 wamezuiliwa kupewa matokeo yao kwa kosa walilolisababisha wenyewe viongozi wa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM).
Kozi za Wahandisi (Engineering) katika chuo kikuu cha Dodoma ada yake ni 1,500,00/= na wanafunzi wote waliomaliza mwaka huu wanalipiwa asilimia mia moja(100%), Hii inamaanisha wanalipiwa ada yote na Bodi ya mikopo ya elimu ya juu.
Uzembe walioufanya Chuo kikuu cha Dodoma ni kwamba waliiambia bodi ya mikopo mwaka 2010, kuwa ada kwa wanafunzi wanaosomea kozi za uhandisi ni 1,200,000/= badala ya 1,500,000/=. Huu ni uzembe wao kwani kama wangeiambia bodi ya mikopo ada kamili, hili tatizo wala lisingetokea na badala yake wanaadhibu wanachuo waliomaliza kwa kuwazuilia matokeo yao.
Mkuu wa chuo alipopigiwa na mwandishi wetu alitoa maneno ya jeuri kwa kusema mwanafunzi ambaye hatalipa hela iliyobakia yaani 300,00/= basi atakuwa amejifukuzisha chuo
kwa ushahidi kwa hili ona mwenyewe jinsi wanafunzi hao walivyoandikiwa kwenye matokeo yao.
Majibu ya Computer engineering bofya HAPA
Majibu ya Telecommunication engineering bofya HAPA
Majibu ya Software engineering bofya HAPA
Tunalaani vikali kwa kuzuiliwa kwa matokeo ya wanafunzi hawa ambao hawana hatia na tunaiomba serikali ifuatilie suala hili ili kuwaepusha wanafunzi hawa kufukuzwa chuo, na waliohusika na uzembe huu wachukuliwe hatua kali za kisheria
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment