Takribani wiki sasa kumekuwa na
taarifa zinazoeleza kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu hayuko
sawa katika mahusiano yake ya kimapenzi na nguli wa Bongo
Fleva, Diamond Plutnumz….
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu na
Wema, imefika mahali Wema anajuta kuwa na Diamond kwa sababu
ya kuandikwa kwa mambo mengi yasiyo na ukweli na
yanayomfedhehesha moyoni….
Rafiki huyo amedai kuwa mara kwa
mara Wema amekuwa akijiuliza sababu ya kuandikwa taarifa
mbalimbali zisizo na kichwa wala miguu ambapo mwisho wa yote
hupata jibu ni kwa sababu ya kuwa na mahusiano na Diamond….
“Wakati mwingine anasema angelijua
bora angebaki bachela kwani kuna kikundi cha watu hakipendi
kumuona akiwa na Diamond hivyo kinafanya kazi ya kumzushia
taarifa zisizoeleweka kila mara kwa lengo la kumshushia
hadhi,” kimesema chanzo hicho
Mwandishi alipokiuliza chanzo hicho ni kwa kiasi gani Wema anamwamini Diamond kilisema:
“Ukweli ni kwamba Wema anampenda
sana Diamond lakini hamwamini kwa sababu wakati mwingine
taarifa zinazoandikwa magazeti hutolewa na Diamond mwenyewe, hali
hiyo inampa wakati mgumu sana Wema kujua ashike wapi na
wapi apaache,”
“Unajua Diamond haaminiki, unaweza kukuta Wema anagombana na watu kumbe mtoa taarifa ni Diamond mwenyewe.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment