Tukio la kudhihirisha kwamba wawili hao ni wapendanao lilitokea juzikati walipokuwa kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta katika Mikoa ya Iringa na Morogoro ambako paparazi wetu aliwafuatilia hatua kwa hatua.
Chanzo chetu kilicho karibu na wawili hao kilipigilia msumari wa uwepo wa penzi motomoto kati ya wawili hao kwa kudai hata ukaribu wa msanii Jux na Vanessa ulioripotiwa hivi karibuni katika vyombo vya habari, ulikuwa ni upambe tu kwa Dimpoz.
“Jux alikuwa mpambe tu kwa Dimpoz wala hakuwa na uhusiano na Vanessa kama wengi walivyokuwa wakifikiri,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya paparazi wetu kuwafotoa picha
kibao zinazowaonesha wawili hao wakipeana kampani ya karibu kwa nyakati
tofauti katika ziara hiyo, alimvaa Dimpoz na kumuuliza kama ndiyo
ameamua kujisevia moja kwa moja au vipi, msikie alichojibu:
“Ujue kuna vitu unaweza kujitahidi sana kubishana na watu lakini kuna
muda inabidi uwe mpole tu kama hii ishu yangu na Vanessa maana
walishaongea sana juu ya uhusiano wetu, sasa nashindwa hata namna ya
kumwepuka.“Hatujawahi kugombana hata siku moja na sina jinsi ya kuepuka kufanya naye chochote maana kama ishu ya mapenzi kati yetu ipo wazi na hakuna jipya ambalo naweza kusema watu wakanielewa,” alisema Ommy Dimpoz.Alipoulizwa Vanessa kuhusiana na uhusiano wao, aliishia kucheka tu na kudai hakuwa na cha kuzungumza.


No comments:
Post a Comment