CHELSEA YANG'AA, PSG YAIBANJUA BARCELONA,, PATA MATOKEO HAPA ZAIDI


CHELSEA imepata ushindi wa ugenini katika Ligi
ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuifunga Sporting
Lisbon ya Ureno bao 1-0, wakati Manchester City
imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na AS Roma
ya Italia usiku huu.
Katika mchezo wa Kundi G, bao la Nemanja
Matic dakika ya 34 limemfanya kocha Jose
Mourinho aitambie timu ya nchini kwake,
Sporting.
Uwanja wa Etihad, Sergio Aguero alitangulia
kuifungia City kwa penalti dakika ya nne kabla ya
mkongwe Francesco Totti kuisawazishia Roma
dakika ya 23 katika mchezo wa Kundi E.
Bao pekee la Thomas Mueller dakika ya 22
limeipa Bayern Munich ushindi wa 1-0 ugenini
dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika mchezo
mwingine wa Kundi E. mchezo mwingine wa
kundi hilo usiku huu, Schalke 04 imelazimishwa
sare ya 1-1 nyumbani na Maribor.
Kundi F, PSG imeichapa FC Barcelona mabao 3-2,
mabao yake yakitiwa kimiani na David Luiz
dakika ya 10, Marco Veratti dakika ya 26 na
Blaise Matuidi dakika ya 54, wakati mabao ya
wageni yalifungwa na Lionel Messi dakika ya 12
na Neymar dakika ya 56.
Mchezo mwingine wa Kundi hilo, APOEL Nicosia
imelazimishwa sare ya 1-1 na Ajax nyumbani bao
la wenyeji likifungwa na Manduca dakika ya 31
na la wageni likifungwa na Lucas Anderson
mapema dakika ya 28.
Kundi H, BATE Borisov imeichapa 2-1 Athletic
Bilbao nyumbani mabao ya washindi yakifungwa
na Denis Polyakov dakika ya 19 na Karnitskiy
dakika ya 41, wakati bao la wageni lilifungwa na
Aritz Aduriz dakika ya 45.
Shakhtar Donetsk imelazimishwa sare ya 2-2
nyumbani na FC Porto, mabao ya wenyeji
yakifungwa na Alex Teixeira dakika ya 52 na Luiz
Adriano dakika ya 85, wakati ya wageni yote
yamefungwa na Jackson Martinez dakika ya 89
kwa penalti na 90.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger