KUFUATIA madai ya hivi karibuni ya mkongwe wa filamu
Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ kuwa baadhi ya waigizaji hawana sifa za kuwa
wacheza sinema zaidi ya kuuza sura, msanii Yusuph Mlela amempa dongo
zito akisema licha ya umri kuwa mkubwa, pia ana matatizo flani
yanayomsumbua.
“Nora naona siyo kosa lake kwani alishaugua yule, isitoshe
ameshakuwa bibi hivyo nimemsamehe na sina tatizo naye kwani najua,
lingekuwa jambo la maana kama angetufuata na kutushauri kama mkongwe
lakini si kwa njia aliyofanya,” alisema Mlela.
Hivi karibuni Nora aliwataja mastaa wenzake wa filamu akiwemo Mlela,
Chuchu Hans, Steve Nyerere, Kajala na Batuli akisema hawawezi kazi zaidi
ya kuuza sura tu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment