Mwanaume
mmoja mkoani Katavi anasakwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa
kumpiga nyundo kichwani kisha kuufungia mwili wa marehemu ndani ya
nyumba.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema tukio hilo
lilitokea kijijini hapo Septemba 14, mwaka huu saa 1.30 asubuhi ambako
mwanamke aitwaye Bernadeta Bwetel (38) mkazi wa Kijiji cha Uruwila
Wilaya ya Mlele aliuawa.
Alisema
kabla ya kifo hicho, enzi za uhai wake mwanamke huyo alikuwa akiishi
pamoja na mume huyo na watoto wao wawili lakini mume wa marehemu alikuwa
na mazoea ya kumpiga mara kwa mara.
Kidavashari
alisema siku ya tukio, majirani zao Raphael Antony na Albert Mayamba
wakielekea shambani walipita jirani na nyumba ya marehemu, walishtushwa
na hali ya hapo ilivyokuwa, tofauti na siku zote ambazo huwa wanaikuta
familia hiyo ikiwa hapo nyumbani na kuhisi kuna tatizo.
Majirani hao walikwenda kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji, ambaye aliongozana nao hadi kwa Mtendaji wa Kata, Didasi Buyaga.
Alisema
baada kufika nyumbani kwa marehemu, walikuta mlango umefungwa kwa kamba
kama ishara ya kuonyesha ndani ya nyumba hiyo hakuna mtu.
“Walipiga hodi lakini hawakujibiwa ndipo walipoamua kuvunja mlango na kuingia ndani na kukuta mwili wa marehemu ukionekana alipigwa na kitu kizito kichwani kinachodhaniwa kuwa ni nyundo lakini hawakumkuta mumewe wala watoto na hadi sasa hawajulikani waliko,” alisema.

No comments:
Post a Comment