WASTARA: WASANII TUNA UMAARUFU MAANDAZI, SOMA ZAIDI HAPA

Muuza sura wa sinema za Kibongo, Wastara Juma amesema yupo kwenye mikakati mizito ya kufanya mapinduzi kwenye tasnia ya filamu na kutambulika kimataifa na ndiyo sababu ya kuanzisha Timu Wastara.
Muuza sura wa sinema za Kibongo, Wastara Juma.
Akipiga stori na paparazi wetu, Wastara ambaye aliitendea haki sinema ya Shaymaa, alisema soko la filamu Bongo bado lipo chini sana kwani wasanii wengi wanajivunia kwa kujulikana majina bila manufaa ya kazi zao, tofauti na nchi za nje ambao wasanii wake wanatambulika kwa kazi zao.
“Wasanii wa Kibongo tuna umaarufu maandazi, tunajinadi kwa majina siyo kazi ndiyo maana utakuta mtu ana umaarufu mkubwa lakini kazi zake huzijui, madhumuni yangu ya kuanzisha hii timu ni kwa sababu nataka kupambana niitoe nchi yetu kimasomaso na kukubalika kimataifa,” alisema Wastara.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger