Jamani mimi nina Kaka yangu Mmoja ambaye ni mtu wa makamo hivi.
Huyu kaka aligundulika kuwa ana maambukizi ya virusi vya ukimwi mwaka 2005 na tangu wakati huo amekua akitumia dawa za kupunguza makari ya virusi vya ukimwi kwa maana kabla ya kugundulika aliugua sana.
Tatizo linalo nitatiza ni kwamba siku za hivi karibuni amepata kabinti kenye umri kati ya miaka 19 - 20 hivi, amekua akishiriki nacho tendo la ndoa kwa takribani kama mara mbili kwa siku ambazo nimeshuhudia binafsi.
Ukweli ni kwamba baada ya kumuuliza kaka ni kwamba kweli anakula mzigo ila akajitetea kua anatumia Kondom.
Sasa kinachonisikitisha ni kua hata kama wanatumia kondom, lakini yule binti hajui kuwa kaka ameathirika, hivyo ninashaka kua siku moja wanaweza kujikuta wanakula mzigo bila kinga.
Ninachoomba kwenu ni ushauri je nifanyaje kuhusu hili? Kwa maana naona njia ya kumuokoa huyu binti ni kumuambia ukweli ili kama atapenda achukue tahadhari stahiki. Binti sijazoeana naye na binafsi sipendi kumkera kaka yangu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment