Siku za hivi karibuni rapper mwenye asili ya Kenya na Tanzania Prezzo alitweet kuwa anaenda mahakamani huko Kenya lakini hakuweka wazi alikuwa anakabiliwa na kesi gani.
Yawezekana ukawa unashangaa kusikia story kila kukicha juu ya king wa bling ana date na warembo wengi kwa wakati mmoja, mara Goldie (marehemu), mara Huddah, mara Diva, na jana tumesikia ameonekana akikiss na mrembo Victoria Kimani. Well! Prezzo alikuwa na mke lakini ndoa yao imetenguliwa rasmi na mahakama kuu ya Nairobi.
Kwa mujibu wa mtandao wa standard media wa Kenya, aliyekuwa mke wa CMB Prezzo Daisy Jematia Kiplagat alifungua kesi ya kudai talaka mwezi May (2012) kutokana na sababu kadhaa ambazo amezitaja.
Daisy ameiambia mahakama kuu ya Nairobi kuwa aliyekuwa mume wake Prezzo alikuwa akifanya uzinzi na wanawake mbalimbali, amekuwa akimpa maneno ya matusi yaliyomsababishia stress, pia amekuwa akimdhalilisha na kushindwa kutimiza majukumu yake ya kuihudumia familia.
Ameendelea kusema Prezzo alikuwa akileta marafiki zake nyumbani na kufanya mambo yao ikiwa ni pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya mbele ya mke wake na mtoto.
Taarifa iliyotolewa na hakimu wa mahakama kuu ya Nairobi imeendelea kusema kuwa Daisy alilalamika pia kuwa CMB Prezzo aliamua kuwa anaondoka kwenda kula bata, kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya na marafiki zake na kumuacha yeye akilea mtoto wao aitwaye Zahrie peke yake bila kutoa huduma yoyote.
Wakati Daisy anafungua kesi ya kudai talaka, alisema Prezzo alihamia kwa mama yake baada ya mapambano ya matusi baina yao, na wiki moja baadaye Daisy aliona habari gazetini kuwa muwewe kipenzi ana mahusiano na mrembo mwingine aitwaye Joy Wanjohi.
Hakimu wa mahakama kuu ya Nairobi aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo Luka Kimaru alisema kutokana na sababu zilizotolewa na Daisy ambazo si nzuri kwa afya ya mafanikio ya ndoa, mahakama hiyo haina chaguo zaidi ya kuitengua ndoa hiyo, hivyo sasa king wa bling ni official single.
Prezzo na Daisy walihalalisha ndoa yao mwezi December (2008) ambayo iliwaletea mtoto wa kike aliyezaliwa March (2009) na waliacha kuishi pamoja toka mwaka (2011) kabla ya ndoa yao kutenguliwa na mahakama kuu ya Nairobi.
No comments:
Post a Comment