"KAMA NINGEKUWA RUGE NINGEMPIGIA MAGOTI JAYDEE NA KUMWOMBA MSAMAHA"....SEBO

Katika kipindi cha Sun Downer cha Magic FM, mtangazaji huyo amesema kwamba shangwe zilizolipuka mara baada ya Jaydee kutajwa kuwa miongoni mwa wanaowania tuzo ya msanii bora wa kike ktk tuzo za KTMA, ni ishara ya mwanadada huyo kukubalika ktk jamii. Mtangazaji huyo amesema kwamba Jaydee ni mwanamke mwenye uthubutu ktk harakati za kuyasaka maisha na kwamba yeyote mwenye nia ya kukwamisha jitihada zake aibu na iwe juu yake. Ameongeza kuwa kukubalika kwa mwanadada huyu pia kulidhihirika pale ambapo watazamaji ktk tukio hilo walipomshinikiza Meneja wa msanii huyo (Gadna) kutaja kiingilio na tarehe ya maadhimisho ya miaka 13 ya Jaydee ktk uga wa muziki. Hivyo, Sebo anaona ni vyema Ruge akajishusha na kumaliza tofauti zake dhidi ya Jaydee.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger