Hali hiyo, ilijitokeza wakati Lissu alipokuwa akitoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni kuhusu muswada huo, kutokana na wadhifa wake kama msemaji wa kambi hiyo kwa Wizara ya Sheria na Katiba.
Lissu, alikuwa akitoa maoni hayo baada ya muswada huo kuwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, ambao unapendekeza marek
ebisho ya sheria tatu.
Sheria hizo, ni Sheria ya Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Sura 292, Sheria ya Tume ya Kurekebisha Sheria, Sura ya 171 na Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298.
Malumbano kati ya Lissu na Spika Makinda, yalianza wakati Mbunge huyo alipokuwa akisoma maoni ya Upinzani, aliilaumu CCM kwa kutumia vibaya vifungu 115 (1) (a) vya Sheria ya Uchaguzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa na kifungu 111 (1) (a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.
Alisema CCM imekuwa na utamaduni mbaya wa kuwarubuni wanachama wake kufungua kesi za uchaguzi dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani.
“Kwa kutumia vifungu hivyo vya sheria, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimejenga utamaduni mbaya wa kurubuni wapiga kura ambao ni wanachama wa CCM kufungua mashauri ya uchaguzi mahakamani dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani waliochaguliwa katika uchaguzi. “Katika kesi hizo, CCM na au wagombea wake walioshindwa wamekuwa wakilipia gharama zote za kuendesha kesi hizo, ikiwa ni pamoja na kuwalipa mawakili na gharama za usafiri, chakula na makazi ya wanaofungua kesi hizo na mashahidi wao,” alisema.
Wakati akiendelea kutamka maneno hayo, Spika Makinda alimkatisha akimweleza kuwa kinachojadiliwa ni sheria na siyo CCM.
“…Mheshimiwa Tundu Lissu hapa tunazungumzia sheria siyo CCM… utaandika sheria kwa kuandika CCM kweli?” alisema na kumtaka Lissu kufuata utaratibu.
Hata hivyo, Lissu alisema anachofanya ni kuzungumzia sheria na upungufu ambao umekwisha kujidhihirisha.
“Mheshimiwa Spika, mimi nazungumzia sheria hii na upungufu ambao umekwisha kujitokeza…,” alisema.
Hata hivyo, Spika alimkatisha na kumuamuru akae. Makinda aliendelea kumweleza Lissu kwamba, kilichokuwa kinafanywa ni kutunga sheria na kwamba masuala ya siasa yafanyiwe kwenye majukwaa.
“Najua Tundu Lissu, anazifahamu kanuni na taratibu…lakini akiamua kuzikunja anazikunja,” alisema Makinda na kumtaka Lissu aendelee kusoma hotuba yake ingawa hakusema ayafute maneno hayo.
Pengine kwa kuona hakutakiwa kuyafuta maneno hayo, Lissu aliendelea kusoma hotuba yake ambayo kwa kiasi kikubwa iliishutumu CCM kwa kutumia vibaya sheria hizo.
Alisema baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, CCM iliwafungulia kesi wabunge 14 wa Chadema na kati ya hao wabunge 11 walifunguliwa na wapiga kura wanachama wa CCM.
Alisema CCM pia iliwafungulia kesi wabunge watatu wa NCCR-Mageuzi, huku kesi zote hizo zikifunguliwa na wanachama wa CCM.
Alisema kesi zote, zilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
Aliwalaumu wakuu wa CCM, Katibu Mkuu wa zamani, Yusufu Makamba na Katibu Mkuu wa sasa, Abdulrahman Kinana, akidai wote kwa nyakati tofauti waliandika barua za kuelekeza kufunguliwa kesi hizo.
Lissu aliilaumu Serikali kwa kutowasilisha bungeni marekebisho ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kupiga marufuku mpiga kura kufungua kesi dhidi ya mbunge aliyeshinda uchaguzi, kwa kuzingatia kutupiliwa mbali na Mahakama ya Rufani kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM kupinga ushindi wa Godbless Lema kama Mbunge wa Arusha Mjini.
“Kawa maneno mengine, kwa mujibu wa uamuzi wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Desemba 20, 2012, katika Shauri Namba 47 la 2012 kati ya Godbless Jonathan Lema dhidi ya Mussa Hamisi Mkanga & wenzake wawili, wapiga kura anmbao haki zao kama wapiga kura hazikuathiriwa na matokeo ya uchaguzi husika, hawana haki ya kulalamikia matokeo ya uchaguzi huo.
“Hivyo Serikali hii ya CCM, ingeleta kama muswada huu mapendekezo ya marekebisho ya kifungu cha 111 (1q) (a) x cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na kifungu 115 (1) (a) cha Sheria ya Uchaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, ili kuviwianisha vifungu hivyo na uamuzi huu wa Mahakama ya Rufani,” alisema.
CHANZO MTANZANIA
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA) jana ‘alimtunishia msuli’ Spika wa Bunge, Anne Makinda wakati wa kujadili Muswada wa Sheria wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment