UPDATE: KESI YA LWAKATARE INASIKILIZWA SASA HIVI SAA NANE MCHANA...!!


Kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Muganyizi Lwakatare ya kujaribu kumwekea sumu Dennis Msaki, kwa sasa imesimama mpaka saa nane mchana baada ya waliofika kumtolea dhamana kukosa baadhi ya vielelezo hivyo kwenda kuvifuatilia. Baadhi ya wanachama wa Chadema kwa sasa wapo nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakisubiri hiyo saa nane ili wajue hatima ya kiongozi wao. Mwandishi wetu aliyepo mahakamani hapo alipoongea na wanachama hao wanadai kuwa leo lazima kieleweke na watahakikisha wanaondoka na kiongozi wao maana amesota sana rumande.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger