OBAMA AMALIZA ZIARA YAKE NA KUREJEA MAREKANI


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Nyuma yao ni Mama Salma Kikwete na Mama Michelle Obama pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na IGP Saidi Mwema . Kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu ya Marekani (White House) Balozi Capricia Marshall. Ziara ya Rais Obama nchini imetajwa kuwa moja ya ziara za viongozi wa nje zilizofanikiwa sana, ambapo maelfu ya Watanzania walijitokeza kumlaki na kumuaga.
 Rais Barack Obama akiagana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa Ilala pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao
 Rais Obama na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One
 Rais Obama na mkewe wakipunga mikono kuaga Watanzania
 Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiaga wageni wao
Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Adam Malima (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe  Alfonso Lenhardt wakipungia kuaga wageni wao

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger