WINNIE MANDELA AELEZEA MACHUNGU ANAYOPATA KWA KUUGUA MANDELA.


Winnie Mandela amebainisha maumivu makali anayohisi kumwona mumewe wa zamani Nelson anateseka hospitalini, akisema ataendelea kumpenda wakati wote licha ya kuachana kwao.
 
Pia alisema kwamba anafurahia uhusiano wa karibu na mke wa pili wa mpinga ubaguzi wa rangi huyo, Graca, na kutania kwamba wanamchukulia kama 'mume wetu'.
 
Wanawake hao wawili wamekuwa kando ya kitanda cha Mandela kwa wiki nne zilizopita huku akiendelea kutibiwa maambukizi katika mapafu kwenye hospitali moja mjini Pretoria.
 
Winnie aliachana na rais huyo wa zamani mwaka 1996, lakini wawili hao wameendelea kuwa karibu kufuatia familia yao pana.
 
Alipoulizwa kama bado anampenda, alisema: "Nitampenda milele, ni baba wa watoto wangu... Hakuna kilichobadilika sababu alifunga ndoa na mtu mwingine.
 
"Hakuna mama anayeweza kusema wanawachukia wapenzi wao bila kujali tukio gani la kijamii lililo kati yao."
 
Pia alisisitiza kwamba anaelewana vema na Graca, ambaye aliolewa na Mandela mwaka 1998.
 
"Namwita mdogo wangu na ananiita dada yake mkubwa, tunashirikiana kila kitu," alisema Winnie. "Anapoongea na mimi, anazungumzia kuhusu 'mume wetu".
 
"Ni familia moja, wote tuko kwenye hali moja kiroho."
Mwanasiasa huyo moto alikanusha vikali ripoti kwamba ndugu  wa Mandela wamekuwa wakilumbana kumuweka au kutomuweka kwenye mashine ya kupumulia.
 
"Ilikuwa ni upuuzi kushauri kwamba tunahitaji kufanya uamuzi kuondoa mipira hiyo," alisema Winnie.
 
"Unaposikia waumini wakisema wanaiombea familia kutochomoa mipira hiyo, nafikiri kwamba hilo limefika mbali kidogo."
 
Binti yake Zindzi aliongeza: "Watu wanaposema, "Familia hiyo lazima isalimu amri" - kusalimu amri kwa kipi? Ni kati yake na muumba wake, haituhusu kwa namna yeyote ile."
 
Winnie pia alikuwa na maneno makali kwa Rais Jacob Zuma na chama tawala cha ANC kwa kupiga picha na Mandela anayeteseka mwezi Aprili.
 
Mzee Mandela mwenye miaka 94 alipigwa picha akiwa mwenye afya tete, akiwa amezungukwa na Zuma na maofisa wengine, na Winnie alisema kwamba picha hiyo ilithibitisha kuwakera ndugu.
 
Barack Obama alilazimika kufuta mkutano aliopangiwa kukutana na kiongozi huyo wakati wa ziara yake Afrika Kusini ambayo ilihitishwa juzi.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger